THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MTANDAO WA JUMIA WAZINDUA CODES ZA PUNGUZO LA BEI.

 Meneja Mkazi wa Mtandao wa JUMIA, Lauritz Elmshauser akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
wakati wa kuzindua punguzo la bei kwa watumiaji wa mtandao wa  watakao nunua bidhaa kupitia JUMIAAPP iliyo kwa kutumia simu zao za mkononi. Watembeleaji wa Mtandao wa JUMIA wenye JUMIAAPP watapunguziwa shilingi 5,000 kwa kila bidhaa atakayokuwa amechangua kununua ila bidhaa hiyo iwe kuanzia kiasi cha shilingi 20,000.

 Elmshauser amesema  watumiajia wa mtandao wao wa JUMIA wenye JUMIAAPP watatakiwa kujaza codes za mtandao huo ambazo ni JUMIAAPP na kujipatia punguzo la bei kwa bidhaa watakazokuwa wamenunua kwa kutumia mtandao wa JUMIA.
Kulia ni Meneja Mkazi wa Mtandao wa JUMIA, Radoslam Mikolaj na Kushoto ni Meneja wa Bidhaa na Masoko wa Mtandao wa JUMIA, Heriath Mgongolwa.
Amesema kuwa mtandao huo wa JUIMIA umekuwa ukiwasaidia sana watu kwa kutoa ajira pamoja na wale wasio kuwa na muda kuwapunguzia usumbufu wa kubeba mizigo kwani mteja anafikishiwa bidhaa yake mahali alipo.
Meneja wa Bidhaa na Masoko wa Mtandao wa JUMIA, Heriath Mgongolwa akionesha Codes za punguzo la bei kwa watumiaji wa mtandao wa JUMIA  unaounganisha wateja na wauzaji pamoja kwaajili ya kufanya biashara ya mtandao ambapo mtumiaji wa Mtandao huo atanunua bidhaa kwenye mtandao na kufikishiwa bidhaa hiyo ndani ya siku tatu. Kulia ni  Meneja Mkazi wa Mtandao wa JUMIA, Lauritz Elmshauser.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Hiyo kampuni inajishughulisha na biashara ya aina gani maana mmewwka punguzo tu kwa bidhaa ipi? Naomba msaasada wa kiufahami