Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, linawashikilia watu wawili ambao ni Mme na Mke kwa tuhuma za matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha za moto katika maeneo tofauti tofauti jijini Dar es salaam.

Watuhumiwa hao ambao wametambulika kwa majina ya Bakari Abdallah (40) na Sihaba Omary (28) wakazi wa Vijibweni, Kigamboni walitiwa mbaroni mnamo tarehe 23 Septemba mwaka huu na Kikosi Maalum cha Jeshi hilo cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha.
Akizungumza mbele ya wanahabari, Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro, alisema kuwa mnamo tarehe 26 Septemba mwaka huu Askari walifika nyumbani kwa watuhumiwa hao na kukuta bastola aina ya "Browning" yenye usajili namba CAR A081900 ikiwa na magazine mbili na risasi tano pamoja na simu aina ya Nokia Lumia ambayo inadaiwa kuwa iliporwa katika matukio ya unyang'anyi.
Watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya oparesheni ambazo zimefanyika maeneo mbalimbali na mafanikio yake leo jijini Dar es Salaam. ambapo Jeshi hilo lilifanikiwa kumtia mbaroni mtu mmoja kwa tuhuhuma za ujambazi wa kutumia silaha za moto.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro akionesha kwa wanahabari silaha zilizokamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro akionyesha gari aina ya Verosa likiwa limesheheni magunia saba za bangi leo iliyokamatwa hivi karibuni jiji Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha gari aina ya Noah ikiwa wan a magunia ya bangi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha namba za gari za bandia ambazo zimekuwa zikitumiwa na waharifu leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Bange mbona chakula jamani, isitoshe ni tiba nzuri tu medical marijuana.Ni juzi The Game amewekeza 100mil ktk biashara yake ya bange huku akitafuta business partner......isitoshe hakuna hata andiko lolote currently hapa kwetu lenye kuonesha bange inaathiri au imeathiri kwa kiasi gani jamii ya waTz.

    ReplyDelete
    Replies
    1. You must not be serious.kwa hiyo kwa upeo wako bangi ni salama kwakua imehalalishwa kwenye baadhi ya nchi?

      Delete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...