Na Shamimu Nyaki-WHUSM  
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura ametoa agizo kwa wasanii nchini kuhakikisha wanasajili kazi zao katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili watambulike kwa mujibu wa Sheria.
Agizo hilo amelitoa jana Jijini Dar es Salaam  alipokuwa anazindua Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Taifa la Sanaa (BASATA) ambapo amewaahidi wasanii kuwa wakijisajili watatambulika  na itakuwa rahisi kwa Serikali kujua changamoto wanazozipata na kuzitatua kwa urahisi.
“Napenda mtambue kwamba suala la Urasimishaji linakwenda sambamba na uwepo wa Haki Miliki ya kazi za ubunifu, nawashauri mtunze Haki Miliki zenu na msiziuze na wale wabunifu  wapya na ambao hamjasajili kazi zenu nawaomba mfanye hivyo ili kuepuka uharamia”.Alisisitiza Mhe. Anastazia.
Aidha Mhe.Naibu Waziri amewaomba wadau wote wa Sanaa kutoa maoni yao katika kuboresha tasnia hii yenye kubeba maeneo kama Muziki, Filamu, Maonyesho, Ususi, na Uchoraji ili kuwezesha tasnia hii kujulikana na  kuboresha mapato ya Wasanii.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza amewataka Wasanii kutunza vibali wanavyopatiwa na Baraza hilo kwani ndio utambulisho wao popote wanapokuwa na inakuwa rahisi wao kusaidiwa wanapopata changamoto.
“Wengi wenu mmejisajili lakini wale wachache ambao bado naomba mfanye hivyo ili sisi tuwatambue na Sheria ya  Haki Miliki pia iwatambue”.Aliongeza Bw.Muingereza.
Naye Msanii wa Uchongaji Bibi Hapiness Mmbaga amewashauri wanawake kupenda fani hiyo na kuacha dhana inayosema kuwa kazi hiyo ni kwa ajili ya wanaume tu kwani ulimwengu wa sasa umebadilika hakuna tena kuchagua aina ya kazi ya kufanya.
Tamasha la siku ya Msanii duniani linaadhimishwa kwa mara tatu mfululizo ambalo linalenga kuthamini mchango wa kazi za Sanaa hapa nchini ambao kauli mbiu yake  ni “Nguvu ya Sanaa”na kilele chake itakuwa ni tarehe 26 mwezi oktoba mwaka huu.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akizungumza na Wasanii kuhusu umuhimu wa kusajili kazi zao wakati wa uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza laTaifa la Sanaa (BASATA) pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production  lililofanyika  Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.



 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza akitoa maelezo mafupi kuhusu siku ya Msanii Duniani wakati wa uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza hilo pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production lililofanyika Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Haak Neel Production Bw. Emmanueli Maendeka akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa Kampuni yake katika uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa  pamoja na Kampuni yake lililofayika Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akiangalia baadhi ya kazi za Sanaa kutoka kwa Wasanii wakati wa  uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Taifa la Sanaa (BASATA)pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production  lililofanyika  Septemba 24 Jijini Dar es Salaam
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akiangalia baadhi ya kazi za Sanaa kutoka kwa Wasanii wakati wa  uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akimkabidhi Cheti cha ushiriki  Bw.Adrian Nyangamale Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi katika uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza laTaifa la Sanaa (BASATA)pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production  lililofanyika  Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...