Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani (kushoto) akizunumza na viongozi na wadau shirikishi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Rafiki Wildlife Foundation kuhusu Kampeni ijulikanayo kama "Jitokeze Tuongee, Piga Vita Ujangili Afrika na Wizara ya Maliasili na Utalii" iliyoandaliwa na shirika hilo kwa ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na wadau wengine ofisini kwake Dar es Salaam jana, tarehe 21 Septemba, 2016. Kampeni hiyo imepangwa kuzinduliwa Jijini Arusha tarehe 07 Oktoba, 2016. Kulia ni mdau wa kampeni hiyo ambaye pia ni Mbunge Mstaafu wa Viti Maalum , Al-Shaymaa Kwegyir.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizungumza na viongozi na wajumbe shirikishi wa Rafiki Wildlife Foundation ofisini kwake jana. Alieleza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi katika kupiga vita ujangili na kuimarisha uhifadhi wa Maliasili nchini. Alitoa wito kwa watanzania kuwa wazalendo kwa nchi yao na kupenda Malisili za taifa na kujenga utaratibu wa kuzitembelea ili kukuza utalii wa ndani ambao Wizara imejipanga kuuendeleza kuhakikisha unakuwa kwa kasi ili kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa.
Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Rafiki Wildlife Foundation, Mchungaji Clement Matwiga (wa tatu kulia) akizungumza katika kikao hicho, Mchungaji huyo alitoa wito kwa watanzania kuwa mstari wa mbele katika ulinzi wa wanyamapori hususani Tembo na Faru kwa kuwa wana faida kubwa kwao kiuchumi na kijamii, alisema kuwa kwa sasa jamii inaona jukumu hilo ni la Serikali pekee kupitia Wizara ya Maliasili na Taasisi zake jambo ambalo sio sahihi. Akielezea kuhusu kampeni ya "Jitokeze Tuongee, Piga Vita Ujangili Afrika na Wizara ya Maliasili na Utalii" itakayozinduliwa Jijini Arusha na Waziri wa Maliasili na Utalii alisema, itahusisha fursa mbalimbali ikiwemo kutembelea hifadhi ya Taifa ya Arusha kwa ajili ya kuhamasisha utalii wa ndani, Semina mbalimbali kuhusu uhifadhi pamoja na michezo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na wajumbe shirikishi wa Rafiki Wildlife Foundation ofisini kwake jana.(Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii - www.wizarayamaliasilinautalii.blogspot.com)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...