Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuwapokea Madereva kumi (10) waliokuwa wametekwa nchini DRC. Katika maelezo yake Mhe. Kolimba ameishukuru Serikali ya DRC kupitia Ubalozi wake hapa nchini kwa kuonyesha ushirikiano mzuri na kufanikisha kupatikana kwa madereva hao.Kulia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hapa nchini, Mhe. Jean Pierre Tshampanga Mutamba na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samuel Shelukindo. Madereva hao wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam 21 Septemba, 2016.
Balozi wa DRC nchini Tanzania, Mhe. Jean Pierre Tshampanga Mutamba akizungumza kwenye mkutano na wanahabari, ambapo alitumia fursa hiyo kuwapa pole madereva hao kwa mkasa uliowakuta na alisisitiza suala la kutoa taarifa Ubalozini pindi wanapoanza safari kuelekea nchini Kongo.
Mmiliki wa Kampuni ya Simba Logistics, Bw. Azim Mohamed Dewji akiishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ushirikiano mzuri waliouonyesha mpaka kufanikisha upatikanaji wa Madereva hao.
Sehemu ya Madereva hao wakiwasikiliza viongozi waliojitokeza kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Mmoja wa Madereva Bw. Athumani Fadhili akisimulia jinsi tukio lilivyotokea mpaka kuokolewa na Vyombo vya usalama nchini Kongo
Naibu Waziri Dkt. Suzan Kolimba, Balozi wa Kongo hapa nchini Mhe. Mutamba Jean Pierne na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Samweli Shelukindo wakiwapokea madereva hao
Naibu Waziri, Dkt. Susan Kolimba akiwa katika picha ya pamoja na madereva waliokuwa wametekwa nchini Kongo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...