Na Lorietha Laurence.

Wajasirimali na wabunifu wa kazi za mikono nchini wahimizwa kuwa na hatimiliki ili kudhibiti wizi wa kudurufu bidhaa zao unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura alipokutana na kikundi cha wajasiriamali cha Handproduct of Tanzania leo jijini Dar es Salaam.

Mhe. Anastazia ameeleza kuwa endapo kazi za wajasriamali zitalindwa kwa kuwa na hatimiliki itasaidia katika kukuza uchumi wao binafsi na kuongeza pato la Taifa. “Ni muhimu kulinda kazi za wajasirimali kama ambavyo kazi za sanaa ya muziki zinavyolindwa kwa kuwa na hatimiliki ili kuwasaidia katika kulinda haki zao za ubunifu” alisema Mhe. Anastazia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo ameeleza kuwa kukosekana kwa hatimiliki katika kazi zao kumeleta changanmoto kubwa na bidhaa feki kutoka kwa wafanyabiashara wa nje ambao wamekuwa wakidurufu kazi zao na kuuza bidhaa kwa bei nafuu.

Aidha Bibi. Elizabeth aliongeza kuwa changamoto nyingine ni ukosefu wa eneo la kufanyia maonyesho ya bidhaa zao kitendo ambacho kinasababisha kukosekana na soko lililoimara kwa bidhaa hizo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Wizara Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Bibi. Lilian Beleko amesema kuwa kweli changamoto hizo zipo na wanazifanyia kazi kuwawezesha wajasiriamali hao wa kazi za sanaa na utamaduni ili waweze kufanya kazi zao kiufanisi.

Kikundi cha Handproduct of Tanzania kilisajiliwa mwaka 2006 na kinajumisha wajasiriamali mbalimbali wanaojihusisha na kazi za mikono kutengeneza bidhaa mbalimbali za utamaduni na sanaa katika kuenzi utamaduni wa Mtanzania.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akionyeshwa bidhaa ya vikapu vya asili vilivyotengenezwa kwa kitenge kutoka kwa mjasiriamali Bibi. Flora Mosha wa Nancy Tailoring Mart (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo. 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akionyeshwa vazi lililodariziwa na mjasiriamali ambaye pia ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo leo jijini Dar es Salaam.Picha na: Lorietha Laurence – WHUSM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...