Mapema asubuhi ya leo, watu wanaodaiwa kuwa ni Madalali wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC) wamefika ofisi za Gazeti la kila siku la Tanzania Daima zilitopo katika makutano ya Mtaa wa Mkwepu na Indraghand na kuwatolea vyombo vyote nje kufuatia deni la muda mrefu la kodi ya pango wanalodaiwa bila kulipwa. Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo, Neville Meena amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wako kwenye Msukosuko mkubwa sana sasa ila wanafanya jitihada za kukabiliana na hali hiyo ili kuhakikisha uzalishaji wa gazeti unaendelea kufanyika kama kawaida. 
Sehemu ya Wafanyakazi wa Gazeti hilo wakiwa nje ya Ofisi huku wakitafakari namna ya kufanya.
Vyombo vya Ofisi hiyo vikiwa nje.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...