THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RAIS DKT MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI NA POLE KAGERA KUFUATIA WATU KADHAA KUPOTEZA MAISHA NA NYUMBA KUBOMOLEWA KWA TETEMEKO LA ARDHIWatu kadhaa wamepoteza maisha na nyumba nyingi  Mkoani Kagera zimebomoka baada ya tetemeko la Ardhi lenye nguvu ya 5.7 kipimo cha Ritcher kupita kwenye mikoa hiyo ya Kanda ya Ziwa.
Taarifa zinadai Mji wa Kamachumu Mkoani Kagera ndio umeathiriwa Vibaya na tetemeko hilo, ambapo nyumba nyingi zimebomolewa.

Kiasi cha watu 10 wamepoteza maisha na mamia kujeruhiwa kwa  mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollomi.

Nyumba Moja wapo ambayo imeathirika na Tetemeko hilo lililotokea Muda mfupi uliopita Mjini Bukoba.

Nyumba ikionekana kupata nyufa baada ya tetemeko la Ardhi kuutikisa Mji wa Bukoba hivi Punde

Milango ya Geti katika nyumba hiyo ikionekana kuanguka chini baada ya kukumbwa na dhoruba ya tetemeko la Ardhi, lililotikisa Mji wa Bukoba.
Baadhi ya Nyumba za Wananchi wa Mji wa Bukoba Zikiwa katika hali Mbaya baada ya Tetemeko la Ardhi Kupita.


Gari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mjini 

Bukoba likiwa katika harakati za Uokoaji. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Poleni.
    Ila tuache kutumia mafundi tutumie wahandisi kudizaini nyumba zetu.

    Hatujui lini tetemeko jingine litatokea, linda nyumba yako na uhai wako kwa kutumia wataalam ambao kodi yako ndo inawasomesha.

  2. Anonymous Anasema:

    Poleni sana wana Kagera. Ili ni janga la taifa na tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu. Tunamuomba Mungu awapunzishe kwa amani wale waliotutangulia na kuwapa haueni na matumaini wote waliopatwa na janga hili.