THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

PPF YAWATAKA WASTAAFU KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA UHAKIKI LINALOENDELEA NCHINI.

 

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

MFUKO wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) umewataka wanachama wastaafu wa mfuko huo PPF kujitokeza katika zoezi la uhakiki linaoendelea na kumalizika nchini kote tarehe 28 Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandsihi wa habari leo jijini Dar es salaam Meneja Kiongozi wa Shughuli za Pensheni na Huduma kwa Wanachama, John Mwalisu alisema uhakiki huo hufanyika kila baada ya miaka miwili kwa lengo la kuwa na taarifa sahihi za wanachama wanaolipwa pensheni kupitia mfuko huo.

Mwalisu alisema zoezi hilo la kuhakiki wa wastaafu lililoanza Septemba 12 hadi Septemba 23 mwaka huu katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar ni endelevu na linatarajia kuendelea mikoani kuanzia Septemba 26 hadi octoba 28 mwaka huu.

Alisema katika zoezi hilo kila mstaafu anatakiwa kwenda na nyaraka kamili za uanachama ikiwemo Kitambulisho cha mstaafu cha PPF, picha ndogo ya rangi, nakala ya kati ya kitambulisho cha Taifa au kadi ya mpiga kura, hati ya kusafiria au leseni ya udereva.

Aliongeza kuwa awamu ya pili ya zoezi hilo litahusisha mikoa ya kanda ya kati ambayo ni Morogoro, Dodoma na Singida kati ya tarehe 26 hadi 30 Septemba mwaka huu, wakati katika mikoa ya kanda ya Ziwa zoezi hilo litaanza Octoba 3 hadi octoba 7 ikihusisha mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera.

Katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini zoezi hilo la uhakiki wa wastaafu litaanza octoba 17 hadi octoba 21 mwaka huu na katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha na Kilimanjaro zoezi hilo litaanza Octoba 24 hadi Octoba 28” alisema Mwalisu.

Aidha ,alisema kuwa zoezi la ukakiki wa wastaafu hao kwa mikoa ya ya Dar es salaam, Pwani na Zanzibar limemalizika Septemba 23 mwaka huu na kutoa wito kwa wanachama wastaafu katika mikoani inayofuata kuonyesha ushirikiano katika zoezi hilo la uhakiki.

Naye Meneja Uhusiano Mfuko huo, Lulu Mengele alisema kuwa katika kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi, PPF imeanzisha mfumo maalumu wa kuchangia (WOTE SCHEME) unaohusiha sekta rasmi na isiyo rasmi kwa lengo la kukidhi mahitaji na kutambua mchango wa wanachama katika uchumi wa nchi.

Aliongeza kuwa mfumo huo pia unatoa fursa mbalimbali kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta rasmi kuweza kunufaika ili kuweza kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Akizungumza kuhusu mfuko wa Wote Scheme, Mengele alisema wanachama wa mfuko huo kuwa ni pamoja na wakulima, mama lishe na wajasiriamali wadogowadogo ambapo kiwango cha chini cha kuchangia kwa kila mwezi ni Tanzania shilingi 20,000.

Meneja Kiongozi wa Pensheni na Huduma kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni PPF, John Mwalisu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la uhakiki wa wanachama wastaafu wa mfuko huo leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Uhusiano wa PPF Bibi. Lulu Mengere.
Meneja Uhusiano wa Uhusiano wa PPF Lulu Mengere akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la uhakiki wa wanachama wastaafu wa mfuko huo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bi. Janeth Ezekiel na Meneja Kiongozi wa Pensheni na Huduma kwa Wanachama wa Mfuko huo, John Mwalisu.
Waandishi wa habari wakimskiliza Meneja Uhusiano wa PPF Bibi. Lulu Mengere (hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Shija, MAELEZO.