Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kabla ya kuanza kwa Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongoza Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016.
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akitoa taarifa juu ya  maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu Serikali kuridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. 

SERIKALI YARIDHIA UTEKELEZAJI WA 
UJENZI WA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA
SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. 
Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo (tarehe 29 Septemba, 2016) Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. 
Taarifa ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020. 
Amesema ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati yake Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania. 
Mradi huom kubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikishaka mpuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikaliza Tanzania na Uganda. 
Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa bomba hilo lenye urefu wa kilometa 1,443 linatarajiwa kusafirisha mapipa 200,000 kwa siku ambapo kila pipa litaliingizia taifa Dola za Marekani 12.2. 
Amebainisha kuwa pamoja na kusafirisha mafuta ya kutoka nchini Uganda bomba hilo pia linatarajiwa kusafirisha mafutakutoka nchi nyingine zaJ amhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudani Kusini ambazo zimeonesha nia ya  kusafirisha mafuta yao kupitia bandari ya Tanga. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaja faida nyingine ambazo Tanzania itazipata kutoka na namradi huo kuwa ni kupatika na kwa ajira zaidi ya 15,000 wakati wa ujenzi na ajira 2,000 baadaya ujenzi kukamilika, kuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia, kukuza biashara katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania, kampuni za ujenziza Tanzania kupata kazi za ujenzi. 
Aidha, amesema Tanzania inatarajia kunufaika zaidi kwa kutumia bomba hilo kupitisha mafuta yanayotarajiwa kupatikana katika maeneo ya ziwa Tanganyika na Ziwa Eyasi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, SEPTEMBA  28, 2016  



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Aise Anko hizi L na R mbona zinawapa shida sana watu wako???? Balaza ndio nini sasa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...