THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM LEO


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoka kuangalia sehemu ya kupakulia mafuta kutoka kwenye meli katika bandari ya Dar es salaam leo akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi  Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo  kuangalia sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa   Kampuni ya Ushushaji Mizigo Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016. 
 


Kuna Maoni 5 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  usimtafute mchawi nd rais , hii yote ni watu kuajiriana kindugu / kirafiki/kikabila /kidini na kujuana bila kujali uwezo na ujuzi wa anayeajiriwa, hao wote inaonyesha hawajui wanachikifanya katika kazi zao

 2. mja mjoli. Anasema:

  Jamani, Mbona hawa watu wanafanya upuuzi sana bandarini? Wanafanya kazi kana kwamba ni watoto/wajinga. Systems zao hazifanyi kazi. Ni rahisi sana kwa watu kuiba au kupitisha chochote bila wao hata kujua chochote.

 3. Anonymous Anasema:

  Hii kali. Kweli kuna mwendo.
  Msemaji hapo juu umesema kweli

 4. Anonymous Anasema:

  Hongera Mheshimiwa Rais. Kila Mfanyakazi lazima awe na Mafunzo halali na uajiri ufuate uwezo wa utendaji kutokana na Elimu Husika. Kwa vile kuna Wenye vyeti halali ila hawana uwezo wa kufanya kazi kivitendo.

 5. Anonymous Anasema:

  duhhh kazi kweli kweli, nahisi hapo mjibu maswali alikuwa anatetemekea miguu..hadi mdomo