THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA ENEO LILILOKUWA NA NYUMBA ZA MAGOMENI KOTA, AONGEA NA WAAKAZI WAKE. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Waziri wa Ardhi Mhe John Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Ali Hapi na viongozi wengine akitembelea eneo lililokuwa Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa waliokuwa wakaazi wa  nyumba za Magomeni Kota  Bw. George Abdi wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli akihutubia  alipotembelea na kuongea na wakaazi wa  Magomeni Kota wilaya ya Kinondoni  jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli akimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Mchechu kuendelea kuwatoa wapamgaji wenye madeni sugu kwenye nyumba ya shirika hilo wakati  alipotembelea na kuongea na wakaazi wa  Magomeni Kota wilaya ya Kinondoni  jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
 Wananchi wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mwenyekiti wa waliokuwa wakaazi  wa  nyumba za Magomeni Kota  Bw. George Abdi wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
 Kiongozi wa wakazi wa  nyumba za Magomeni Kota Bi Mwajuma  Sama akiongea machache na kuomba dua  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli   alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016. 
PICHA NA IKULU.


Kuna Maoni 3 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Mradi wa kuwekeza katika kujenga nyumba za kisasa katika miji yetu ili tuishi maisha yenye staha, ni mizuri kabisa na ya kuungwa mkono. Mradi wa kuongeza mabweni Chuo kikuu cha Dar-es-Salaam nao unaleta matumaini ya kupunguza kusomea off campus katika mazingira magumu ya kusomea. Utumiaji wa wataalamu wa ndani na vijana wetu katika miradi hii ya maendeleo ni jambo zuri la kuongeza ajira, na kushirikisha wananchi katika ujenzi na kipato kinachoweza kuchangia maendeleo mengine nchini. Shirika la nyumba likusanye kodi ya pango ili kujiendesha na kupata mtaji wa kuboresha makazi nchini.

  2. Anonymous Anasema:

    Vipi kuhusu kanuni za free fair trade.

  3. Anonymous Anasema:

    Sala ya makonda iko inclusive kwa hadhira yote. Haikumpedelea mkristo kwa kuweka maneno ya kikristo japo yeye ni mkristo, hivo kukaribisha waislam. Na pia haikuweka maneno ya kiislamu hivo kukaribisha wakristo. Huu ndo mfano mzuri wa viongozi wa serikali walioahidi kutobagua dini ya mtu. Niamini nimeona viongozi wanafanya maombi ya jumla halafu watumia sala za dini zao. Hii ni nchi ya kisekyula.