Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 12 Septemba, 2016 anatarajiwa kuwasili Mjini Lusaka nchini Zambia kwa ziara ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zitakazofanyika keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.

Rais Magufuli anafanya ziara hii ya kwanza nchini Zambia akiwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Kamati hiyo inajulikana kwa jina la SADC-Troika.

Dkt. Magufuli alipokea kijiti cha Uenyekiti wa SADC-Troika kutoka kwa Rais wa nne Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika katika Jiji la Mbabane nchini Swaziland tarehe 01 Septemba, 2016.

Katika Ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika watakaohudhuria sherehe hizo zitakazofanyika katika Uwanja wa Mashujaa Jijini Lusaka.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Lusaka



11 Septemba, 2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tangu achaguliwe Raisi wetu Magufuli anatakiwa kutoa kipaumbele kutembelea majirani zetu wa damu Kenya, Uganda ni majirani na tuko katika jumuiya na tuna historia ya ujirani, na hii haiitaji shuruti wala pressure, ni ustaarabu tu na busara ya uongozi.

    ReplyDelete
  2. Ni swali tu Kenyatta alishawahi kuja Tanzania just to visit? Akaacha kazi zake na kuja kutembelea Jirani yake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...