Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q 400 zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Kesho kuanzia saa mbili asubuhi.
“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.
Ndege hizo aina ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja  zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi za jirani zitakapoanza kazi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali  ikipata Saluti ya maji (Water Canon Salutation) mara tu baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali  ikiegeshwa karibu na pacha wake iliyofika wiki moja uliopita katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho na viongozi wengine wakielekea kwenye Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali ilipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho  akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi (kushoto kwake) pamoja na maafisa wengine kutoka taasisi mbalimbali za serikali wakiwa katika Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali  mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa


  1. Jamani hicho kiramani cha Afrika kwenye koti mbona kimekuwa upside down nisameheni kama nimekosea

    ReplyDelete
  2. Piga kazi baba Magufuli, wenye uchungu wa nchi hii tuko nawe kwa kila jambo. Wapiga kelele wakameze viwembe tu kama vipi

    ReplyDelete
  3. HATUTAWAANGUSHA AIR TANZANIA NA NYIE MSITUANGUSHE KWA HUDUMA MBOVU,TUNAHITAJI MABADILIKO YA KWELI,ILIKUWA AIBU TANZANIA NCHI MAARUFU KATIKA AFRIKA KWA UTALII. LAKINI HAINA HATA NDEGE NI AIBU,HAPA TUNAJIFUNZA NINI?? UZEMBE WA SERIKALI YA AWAMU YA NNE KWENDA KUKODISHA NDEGE AIRBUS 320 WAKATI FEDHA HIZO ZINGELITOSHA KUNUNUA NDEGE NDOGO MPYA LAKINI TUMESHIA KUDAIWA MADENI TU NA HASARA YA NDEGE AMBAYO HATA HAIKUFANYA KAZI.MIMI NASHANGAA WASOMI WA TANZANIA HIZO NONDO ZAO NI ZA KWELI? WANAIPELEKA TANZANIA WAPI,MIKATABA MIBOVU KILA MAHALI MIKATABA MIBOVU KILIO CHA KUINGIZA NCHI KWENYE UMASIKINI WAKATI TUNATAKIWA KWENDA MBELE SISI TUNARUDI NYUMA.TUNAHITAJI BAADA YA HAPO NDEGE KUBWA BOIENG 737-800,ILI KUWEZA KUHIMILI USHINDANI.NAWATAKIA KILA LA KHERI AIR TANZANIA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...