Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Septemba, 2016
amemuapisha Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,
Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Bw. Doto M. James aliteuliwa kushika wadhifa huo jana tarehe 31 Agosti, 2016 na amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Servacius Likwelile ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Bw. Doto M. James aliteuliwa kushika wadhifa huo jana tarehe 31 Agosti, 2016 na amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Servacius Likwelile ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi
huo, Bw. Doto M. James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango
(Sera).
Hafla ya kuapishwa kwa Bw. Doto M. James imehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Hafla ya kuapishwa kwa Bw. Doto M. James imehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Aidha, Bw. Doto M.
James amekula kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma, zoezi ambalo limeongozwa
na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
salaam
01
Septemba, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimuapisha Doto James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mipango.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Fedha na
Mipango Doto James mara baada ya kuapishwa.PICHA NA IKULU
MKUU WA NCHI HII PICHA YA LEO NDIYO SAWA, NYUMA YENU HAKUNA WATU WNGINE, HII SASA NAONA MNAKUWA WA KIMATAIFA.
ReplyDeleteDR, JAMESY
Ajira za watoto wa wakulima na wafanyakazi zimesahulika!!! Miezi miwili iliyosemwa imeshatimia!!! Bring back our employment
ReplyDeleteKweli kabisa. Picha ya leo safi sana. Keep it up.
ReplyDelete