Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu
Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania.
Taarifa
iliyotolewa leo tarehe 20 Septemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu
Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.Luteni Kanali
Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu
Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.
Wakati
huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis
Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania
(TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.
Dkt. Hedwiga
Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika
hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Balozi
Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.
Balozi Ladislaus
Columbas Komba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Christopher Celestine
Liundi ambaye amemaliza muda wake.
Halikadhalika,
Rais
Magufuli amemteua Bw. Fidelis Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya
Taifa ya Matumizi ya ardhi kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.Bw. Fidelis
Mutakyamilwa ni Mwanasheria Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa LAPF
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
20
Septemba, 2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...