Na Woinde shizza,Arusha

SHIRIKISHO la wasanii wa filamu jijini Arusha wameshukiwa na neema kutoka kwa Mkuu wa mkoa,Mh Mrisho Gambo kufuatia mkuu huyo kuwahidi kutatua matatizo yao.

RC Gambo ameahidi kuwasaidia wasanii wa filamu Mkoani hapa ambapo amewataka kufika ofisini kwake mapema kesho kwa ajili ya kuwasikikiza na kutatua kero zao.

Akizungumza  leo katika ufunguzi wa Mafunzo yaliyoandaliwa na jiji hilo ya siku mbili yenye lengo la kuwafundisha vijana ujasiriamali na jinsi ya kujikwamua katika umaskini Gambo aliwataka vijana kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na asilimia tano inayo toka serikalini.

" Tunaamini serikali yetu imekusudia kuwasidia wanyonge na wote wenye juhudi katika utafutaji hivyo ni vyema mkachangamkia fursa zitolewazo katika jamii yenu na mjiunge katika vikundi ambapo mtanufaika. alisema Gambo.

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la waigizaji wa filamu jijini Arusha(TDFAA) Isack Chalo alisema tasnia ya usanii mkoani hapo inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo ukosefu wa Eneo la kufanyia mazoezi na Television ya mkoa ya kuonyesha kazi zao.

" Tunatamani kupata eneo la kufanyia shughuli zetu hususani mazoezi kwani tulizoea kufanyia shule ya msingi makubusho ambapo kwa sasa tumefukuzwa , hatuna sehemu ya Uhuru kufanyia mazoezi yetu" alisema Chalo.

Alisema walikuwa wamepanga kujenga Meru Village sehemu ambapo wangepata uwanja mpana wa kufanyia mazoezi lakini hadi sasa hawajafanikiwa kutokana na kukosa sapoti.

"Kama vile wasanii wa Dar es salam walivyopatiwa eneo kule Bagamoyo na sisi tunapenda tukumbukwe katika hili ili tuwe huru katika kufanya shughuli zetu pamoja na pia tuweze kutambulika" alisema.

Aliwataka wana Arusha kununua kazi za wasanii wa Arusha na wasiegemee tu upande mmoja wa filamu za Kikorea ( seasons) wakawasahau watu wa nyumbani jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya wasanii Arusha na Tanzania kwa ujumla.

Naye Mmoja wa wasanii hao Experinsia Musa akisoma risala mbele ya Mkuu wa mkoa alisema pamoja na kupatiwa eneo la kujenga ofisi zao, bado wanakabiliwa na eneo la kilimo na ufugaji kwa wale wasanii wasiokuwa na ajira ili waweze kujiajiri kupitia kilimo na ufugaji.

Wasanii wa mkoa wa Arusha pia walitumia fursa hiyo ya kumkabidhi mkuu wa mkoa,Mrisho Gambo baadhi ya kazi zao ambazo wamezifanya ili na yeye azione na aweze kuwasadia zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiongea na wasanii wa mkoa wa Arusha waliohudhuria semina ya Ujasiriamali iliyofanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi ya Arusha School iliopo jijini humu
Wasanii wa aina mbalimbali wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwa makini

Kaimu Afisa maendeleo ya Jamii Jiji Tajieli Mahega akisoma risala fupi inayoelezea lengo la kuandaa mafunzo hayo kwa wasanii hao
Kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Rebeka Mongi akiwa anaongea na wasanii wa mkoa wa Arusha waliohudhuria mafunzo hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha
 .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...