Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya siku moja ya
kuwajengea uwezo Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya
zote za Mkoa wake kuhusu kusimamia kikamilifu Mpango
mpya wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa bila ya
malipo Kwa watoto wenye Umri chini ya miaka mitano
katika Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa VETA Mjini Iringa, ambapo utekelezaji wake utaanza hivi karibuni
katika Mikoa ya Iringa na Njombe. kulia kwake ni Kaimu Afisa
Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi. Emmy Hudson, anayemfuatia kulia ni
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Richard Kasesela na Mwingine ni
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Nuhu Mwasumilwe.
Wajumbe wa mkutano wakifuatilia Hotuba ya ufunguzi kutoka
kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza kuhusu
usimamizi na ufuatiliaji wa Mpango mpya wa Usajili na kutoa
vyeti vya kuzaliwa bila ya malipo Kwa watoto wenye
Umri chini ya miaka mitano pindi utakapoanza kutekelezwa
katika Halmashauri na Wilaya zote za Mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza akiwa katika picha
ya pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri
za Iringa, Kilolo na Mufindi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...