Kamapuni ya SBC Tanzania Limited, watengenezaji wa vinywaji baridi ya PEPSI, imekabidhi madawati 200 yenye thamani ya Shilingi milioni 22, kwa mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema, ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za kampuni hiyo kuitikia wito wa serikali kuchangia madawati kwa ajili ya kumaliza kabisa matatizo ya madawati mashuleni. 

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya msingi Gogo iliyoko eneo la Chanika, Wilaya ya Ilala, Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Sophia Mjema mbali na kuwashukuru SBC Tanzania Limited kwa msaada huo, alitoa maagizo kwa watendaji wake kuhakikisha kuwa misaada ya madawati wanazoendelea kupokea kutoka kwa wadau mbalimbali zinaelekezwa katika mashule mapya na yale ya zamani yenye mahitaji.

“Nawapongeza SBC Tanzania Limited kwa kuendelea kutuchangia madawati haya. Hili jambo ni jema kwa sababu kampuni hii imeona ni muhimu watoto wetu ambao wako Wilaya ya Ilala wapate madawati, wawezekuwa na elimu bora, waweze kufaulu vizuri ili kesho na keshokutwa wawaajiri wao. Watakapo pata elimu bora, watakapokuwa wataalam wazuri, ni hawa hawa watakao waajiri.

“Vijana wetu wakipata ajira katika makampuni kama ya SBC Tanzania, itatusaidia kuepukana na tabia ya vijana wetu kujiingiza katika uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya. Vijana wetu wakipata elimu bora,watakuwa ni nguvu kazi yenye tija kwa ukuwaji wa uchumi wa taifa letu,” alisema Mjema.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya SBC Tanzania Limited (PEPSI), Bw. Avinash Jha alisema kuwa kampuni hiyo inatambua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya elimu nchini na ndio maana elimu imepewa umuhimu mkubwa katika sera yao ya kuisaidia jamii (yaani Corporate Social Responsibility).

“Mwezi uliopita (Agosti) kampuni yetu kupitia tawi latu la Shinyanga, tulichangia Shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia kutengeneza madawati kwa ajili ya shule za mkoa wa Shinyanga. Mwaka jaana tulichangia madawati 100 kwa Shule za Msingi za Muhimbili na Umoja wa Mataifa huko upanga.

“Ningependa kukuhakikishia, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya, kwamba hata baada ya mchango wetu wa leo, tutaendelea kusaidiana na serikali kadri tunavyoweza kuhakikisha sekta hii muhimu ya elimu inaboreshwa zaidi,” alisema Bw. Jha.

Mkurugenzi huyo aliongeza kwamba kampuni yake inatambua kuwa ili taifa liweze kupiga hatua za kimaendeleo, ni lazima uwekezaji ufanyike katika kuboresha sera na miundombinu ya elimu ili kuzalisha rasilimali watu ya kutosheleza mahitaji ya taifa.

Aliendelea kusema kwamba kampuni ya SBC (PEPSI) ikiwa kama mdau wa maendeleo inatambua kuwa juhudi za wananchi katika kujikwamua katika umaskini hazitafanikiwa kama taifa litashindwa kutoa elimu iliyo bora kwa wananchi wake.

“Kupitia sera yetu ya msaada kwa jamii, kampuni ya SBC (PEPSI) imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika sekta ya elimu. Kampuni yetu pia imekuwa ikitoa nafasi za mafunzo ya kazi “field and internship” kwa wanafunzi zaidi ya 10 kila mwaka ili kuwajenga uzoefu wa kazi,” alisema Bw. Jha.

Aidha, Mkurugenzi huyo alieleza kwamba ni imani yao kuwa mchango waliyotoa itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la upungufu wa madawati katika shule zitakazopata madawati hayo.

“Na kama nilivyo tangulia kusema hapo awali, huu ni mwanzo tu. Tutaendelea kushirikiana na serikali katika kusaidia sekta ya elimu, ikiwa ni pamoja na kuona kuwa kila mtoto anakaa kwemye dawati. Si hapa tu katika wilaya yako ya Ilala, Mheshimiwa Mjema, bali Tanzania nzima.

“Tunafahamu kuwa wanafunzi wanaposoma katika mazingira mazuri hupelekea kuhudhuria vipindi, kuipenda shule, kuelewa vizuri na hatimaye kupelekea kufaulu masomo yao.

“Wananfunzi wanapowekewa mazingira mazuri ya kusomea pia hutoa hamasa kwa walimu kufanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa kwani ufundishaji unakuwa ni rahisi na vivyo hivyo uelewa kwa wanafunzi.

“Hivyo basi, ningependa kutoa wito kwa wanafunzi wayatunze madawati haya ili yaje kuwanufaisha na wenzao watakaokuja siku za usoni na tunawaahidi kuwa tuko pamoja nao katika kutatua changamoto zinazowakabili,”alisema Bw. Jha.
 Ilala District Commissioner Ms. Sophia Mjema (left) and SBC Tanzania Limited Chief Executive Officer Mr. Avinash Jha (right) waves at pupils of Gogo Primary School in Ilala District, shortly after the soft drink bottling company handed over 200 desks worth TShs 22 million to the school.
 Ilala District Commissioner Ms. Sophia Mjema (right) hands over a sample of 200 desks worth TShs 22 million donated by SBC Tanzania Limited (PEPSI), to Gogo Primary School Headmaster Mr. Simon Mdendemi (left). Second right is SBC Tanzania Limited Chief Executive Officer Mr. Avinash Jha, third right is Gogo Primary School Committee Chairperson Ms. Kitu Omary and on her right is Acting Education Officer for Ilala Municipality Ms. Asha Mapunda.
 Ilala District Commissioner Ms. Sophia Mjema (right) applauds after receiving 200 desks worth TShs 22 million donated by SBC Tanzania Limited (PEPSI), to Gogo Primary School in Ilala District, Chanika area. Seated are Gogo Primary School pupils, while standing behind are SBC Tanzania Limited General Manager Johan Voigt (second right), SBC Tanzania Limited Chief Executive Officer Mr. Avinash Jha (third from right) and Acting Education Officer for Ilala Municipality Ms. Asha Mapunda.
Ilala District Commissioner, Ms. Sophia Mjema (left) is welcomed by SBC Tanzania Limited team at a handover ceremony of 200 desks worth TShs 22 million to Gogo primary school. From left after the DC is SBC Tanzania Head of Corporate Affairs Mr. Alexander Foti Nyirenda, followed by the company’s CEO Mr. Avinash Jha, followed by Johan Voigt (General Manager) and Relations Officer Mr. John Msabaha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...