Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, wakijifua kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo. Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville. 
 Kocha wa Makipa wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Muharami Mohammed maarufu kwa jina la Shilton (wa pili kushoto) akiwanoa vijana wake, Kelvin Kayego (kushoto), Ramadhani Kabwili (wa tatu kushoto) na Samwel Brazio kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo. Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville.
 
 Purukushani langoni ambako Dickson Job akiwa hewani akikoa hatari langoni kwake.
 Shughuli ilikuwa kati ya Kelvin Nashot Naftal (kushoto) na Zuberi Rashid Ada.
Madaktari wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Dk. Sheicky Mngazija (kushoto) na Gilbert Kigadye wakifuatilia kwa karibu mazoezi ya timu kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo. Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville.  Picha zote na Alfred Lucas wa TFF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...