Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya mara baada ya kutua leo wakitokea Kigali nchini Rwanda walikopiga kambi kabla ya kuwavaa vijana wenzao wa Congo Brazaville Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Massamba Sebat, Brazzaville.  Timu hiyo imefikia Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini humo. Kikosi hicho kimetua salama salmin kujindaa kuifumua Congo Jumapili. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).
 Kutoa kushoto, Kibwana Shomari, Yohana Mkomola na Rashid Ada wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya mara baada ya kutua leo wakitokea Kigali nchini Rwanda.
 Wakiingia Hotelini.
 Serengeti Boys wakiingia Hotelini.
Makocha wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Muharami Mohammed Sultan maarufu kama Shilton (kushoto) anayewanoa makipa, Kocha Mkuu Bakari Nyundo Shime au Mchawi Mweusi na Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini Brazzaville, Congo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...