Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia 
Nchini(GST) Profesa Abdulkarim Mruma,
Na Sheila Simba,Maelezo.
WAKALA wa Jiolojia Nchini (GST) imezitaka Taasisi za Umma, Wizara na Idara za Serikali kuwatumia Wataalamu wa jiolojia katika shughuli za ujenzi wa ofisi za Serikali Mkoani Dodoma ili kuweza kukabiliana na athari za matetemeko la ardhi yanayotokea mara kwa mara Mkoani humo. 
Wito huo umetolewa leo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Nchini(GST) Profesa Abdulkarim Mruma, wakati wa mahojiano yake na MAELEZO kuhusiana na athari zitokanakazo na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo matetemo ya ardhi hususani katika kipindi hiki ambacho Serikali imepanga kuhamishia shughuli zake mkoani Dodoma. 

“Nashauri Serikali kutuma wataalamu kufanya utafiti ili kuangalia ni maeneo gani yanafaa kujenga ofisi za Serikali na zinatakiwa zijengwe kwa mfumo upi ili ziweze kuhimili matetemeko ya ardhi pindi yanapotokea” alisema Profesa Mruma .Aliongeza kuwa hapo awali ujenzi wa magorofa mkoani humo ilikuwa mwisho ghorofa nne kutokana na mkoa huo kupitia na Bonde la Ufa la Afrika Mashariki ambalo kusababisha matetemeko ya mara kwa mara. 
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa maghorofa Mkoani humo, Prof. alisema magorofa yanayotakiwa kujengwa yawe mapana na yenye kuzingatia ugumu wa nondo, aina saruji inayotumika katika ujenzi na uimara wa jengo husika. “Jengo likiwa nyembamba na refu ni rahisi kupata madhara pindi tetemeko linapotekea hivyo ni vyema watu wafuate ushauri wa wataalamu kabla kufanya ujenzi na pia kuangalia maeneo yanayofaa kwa ujenzi” alisema Prof Mruma.
Aidha ameongeza kuwa majengo yote yatakayojengwa yanatakiwa kuzingatia ubora wa majengo kwa kutumia wataalamu badala ya kujenga bila kushirikisha wataalamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. I believe he is Earthquake Specialist and not Structural Engineer!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...