Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akihutubia wanakijiji cha Kipara Mpakani kabla ya Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Maghembe kukabidhi eneo la hekali 50 kwa kijiji hicho kwa ajili ya huduma za kijamii.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akihutubia wanakijiji cha Kipara Mpakani katika mkutano huo kabla ya makabidhiano.
  Mzee wa Kijiji cha Kipara Mpakani akimshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, kwaniaba ya wanakijiji hicho.

Na Mwandishi Wetu.
SERIKALI imerejesha eneo la hekeli 50 Kwa wananchi wa kijiji cha kipara mpakani kilichopo Kata ya Mwandege,Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ili wajenge huduma za kijamii.

Akikabidhi eneo hilo Waziri wa Maliasi na Utalii Profesa  Jumanne Maghembe aliwaeleza wananchi hao ambo walijitokeza Kwa wingi katika mkutano amesema kuwa wamponge Mbunge  wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kwani amefanya jitihada kubwa za kuhakikisha Serikili inatoa Kwa wananchi eneo hilo.

Amesema kuwa wakati wako Bungeni mbunge huyo pamoja na baadhi viongozi wa kata  hiyo walikwenda Bungeni na kuiomba Serikali kuwapa eneo hilo ambapo lilikuwa pori tengefu la  maliasili ili wananchi wa kata ya Mwandege waweze kujenga Masoko.Shule,na miundombinu mingine.

"Nawapa eneo hili leo kwaniaba ya Serikali kwani najuwa Mh.rais Dkt.Magufuli wakati wakampeni alipita hapa nakuzungumzia eneo hili hivyo tunahitaji mjenge huduma mbalimbali na sio baadae watu wajitokeze na kusema eneo la kwenu."amesema Profesa Maghembe.

Naye Mbunge Ulega akizungumza katika mkutano huo amesema kuwa wananchi hao niwastaratibu kwani.mbali na kukosa maeneo ya kujenga huduma za jamii bado walikuwa wamekituza eneo hilo hadi leo Serikali wanapoamua kuwapa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...