WAJASIRIAMALI nchini wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho mbalimbali yanayoandaliwa na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO),ili kuweza kuzitangaza bidhaa zao na kujifunza mbinu za kuboresha thamani bidhaa wanazozitengeneza.
Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji, amesema maonyesho ya biashara kwa wajasiriamali yana umuhimu mkubwa kwani hutoa fursa ya kipekee kwa kujifunza na pia kutafuta masoko ya bidhaa.
“Maonyesho  ya kikanda yanayoandaliwa na SIDO yanawaleta pamoja wajasiriamali wengi wakiwepo wale wanaotoka nchi za jirani ambao nao huja na bidhaa mbalimbali kuzionyesha na kuzinadi kwenye maonyesho,” Profesa Mpanduji alisema.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maonyesho ya Kanda ya Kusini ambayo yanatarajiwa kufunguliwa kesho jijini Mbeya na kumalizika Oktoba 4, Profesa Mpanduji amewaka wajasiriamali kuchangamkia fursa za maonyesho hayo kuzitangaza bidhaa zao.
“Zaidi ya wafanyabiashara zaidi ya 200 wamethibitisha kushiriki kwenye maonyesho hayo,” alisema na kuongeza kuwa SIDO kwa kushirikiana na wadau wengine imejidhatiti kuhakikisha kuwa bidhaa zinazotengeneza na wajasiriamali wadogo zinakuwa na ubora unaostahili na kushindana kimataifa.
Profesa Mpanduja alisema bidhaa mbalimbali za ngozi, kusindika na mikono zitakuwepo kwenye maonyesho na pia wajasiriamali kutoka nchini Kenya watashiriki.
“Haya ni maonyesho ya 98 na SIDO inayapatia kipaumbele kikubwa kwani yanatoa fursa kwa wajasirialimali kujifunza mbinu na maarifa yakufanya biashara ikiwemo kupata masoko, mikopo na pia namna ya kuboresha bidhaa zao,” alisisitiza.
Alizitaja baadhi ya Taasisi za fedha  kama benki za CRDB, NMB, Diamond Trust kuwa nazo zitashiriki kwenye maonyesho hayo ya kanda ya kusini ambayo inaundwa na mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa na Njombe.
“Shirika la Viwango nchini (TBS), Mamlaka ya Dawa na Chakula (TDFA) pamoja na Mamlaka ya Biashara nchi (TAN-TRADE) watashiriki katika maonyesho hayo muhimu,” Profesa Mpanduji alisema.
Profesa Mpanduji ametoa wito kwa wajasiriamali  kutoka katika kanda nyingine za jirani kujitokeza na kuchangamkia fursa za maonyesho hayo ya kipekee.
“Ninapenda kupongeza mwamko mkubwa wa wajasiriamali na wanavyotengeneza bidhaa za kiwango cha juu,” alisema na kuongeza kuwa wakati umefika kwa watanzania kununua na kujivunia bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji, akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana kuhusu maonesho ya wajasiriamali kwa kanda ya kusini yanayoanza Mkoani Mbeya kesho ambapo washiriki zaidi ya 200 wamethibitisha ushiriki wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...