Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa Mh.
Mhe. Job Ndugai; leo amekuwa miongoni mwa viongozi waliokabidhiwa Kitambulisho cha
Taifa chenye muonekano mpya, baada ya kutembelea eneo ambapo waheshimiwa
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa wakisajiliwa na
kugawiwa vitambulisho vya Taifa vyenye muonekano mpya.
Akikabidhi Kitambulisho
hicho, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Iramba Magharibi Mhe.
Mwigulu Nchemba; amesema hatua ilivyofikiwa sasa na Serikali ni kuona zoezi la
Vitambulisho vya Taifa linakamilika na kuanza kuwa chachu katika kuleta
maendeleo na suluhisho katika huduma nchini zenye kuhitaji utambuzi.
Amesema Kitambulisho cha
Taifa kina umuhimu mkubwa katika maendeleo, ustawi na usalama wa Taifa; hivyo
hakuna budi kuhakikisha mipango ya utekelezaji inakamilika ili kutoa wigo mpana
wa matumizi ya Vitambulisho pamoja na kuunganisha mifumo ya Serikali
kubadilishana taarifa kwa lengo la kuleta ufanisi zaidi katika utoaji huduma
kwa jamii
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kitambulisho chake; Mh. Spika amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa; na kutoa wito wa kuharakishwa kuunganishwa kwa mifumo mingine ya Serikali na NIDA ili kusaidia Serikali kufikia kwa haraka malengo iliyojiwekea kwa wananchi na kuimarisha ulinzi na usalama wa Taifa
Wengine waliopewa
vitambulisho leo ni pamoja na Mh. Tulia Akson Mwansasu Naibu Spika, Mawaziri
Naibu Mawaziri, wabunge na baadhi ya wafanyakazi wa Bunge
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa Mhe. Job Ndugai
akipokea Kitambulisho chake chenye saini kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba katika makabidhiano mafupi yaliyofanyika Bungeni
Dodoma leo
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa Mhe. Job Ndugai
akiweka saini kitabu cha kumbukumbu baada kupokea Kitambulisho chake Bungeni
Dodoma Leo. Kulia ni Afisa Usajili wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bwana. Khalid
Mrisho.
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati NIDA Bi. Rose Mdami akitoa
maelezo kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa
Kongwa Mhe. Job Ndugai kuhusu shughuli za ugawaji Vitambulisho vya Taifa
zinazoendelea kwa waheshimiwa Wabunge mjini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mhe. Mwigulu Nchemba
Watumishi
wa NIDA wakitoa huduma ya ugawaji vitambulisho vyenye saini kwa Wabunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bungeni Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...