Na Dotto Mwaibale
MATAIFA 54 ya Barani Ulaya siku ya Jumapili hii yatashuka dimbani katika harakati za kuwania nafasi ya kufuzu ili kuungana na mwenyeji nchi ya Urusi katika michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini humo mwaka 2018.
Akitoa taarifa hiyo ya kusisimua kwa mashabiki wa soka nchini Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania,  Zuhura Hanif amesema kuwa hii ni habari njema kwa wateja wetu na watanzania kwani wataweza kufuatilia kwa ukaribu kabisa mechi zote moja kwa moja kwenye runinga zao.
“Michuano ya kuwania tiketi ya kufuzu kwenye kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi mwaka 2018 kwa nchi za Ulaya itakuwa ni yenye ushindani mkubwa ukizingatia ubora wa timu na wachezaji wake. Kwenye michuano hii mashabiki wataweza kujionea moja kwa moja mabingwa watetezi Ujerumani watakapoanza safari yao ya kulitetea kombe hilo kwa kuvaana na Norway. 
Pia macho ya wapenzi wengi wa soka watapenda kuiona Uingereza ikiwa chini ya kocha wake mpya Sam Allardyce watakaposhuka dimbani kucheza na Slovakia.” Alisema Hanif
“StarTimes inayofuraha kuwataarifu watanzania kwamba mechi zote za michuano hii zitaonekana moja kwa moja kupitia chaneli zetu mahususi kabisa za michezo ambazo ni Sports Focus, Sport Arena, World Football, Sport Arena na Sport Premium. 
Tunafahamu ya kwamba soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nchini, na sisi tupo katika kuhakikisha kuwa hilo linawezekana kwa gharama nafuu kabisa.” Aliongezea Hanif
Mabingwa wa kombe la EURO mwaka 2016 timu ya Ureno nayo itashuka dimbani siku ya Jumatatu ya Septemba 5 kwenye mchezo wa kundi B dhidi ya Uswisi jijini Basel bila ya nahodha wake Christiano Ronaldo ambaye bado anauguza jeraha la goti ambalo lilimfanya atolewe kwenye kipindi cha kwanza kwenye fainali za EURO zilizofanyika nchini Ufaransa.
“Michezo na burudani ni maudhui ambayo tunayatilia sana maanani StarTimes na ndiyo maana kila kukicha tunazidi kuongeza zaidi. Wateja wetu kwa malipo ya gharama nafuu kabisa ya mwezi wataweza kutazama mechi zote za michuano hii moja kwa moja kwenye chaneli tano tulizonazo mahususi kwa michezo pekee. 
Ninawaomba watanzania kuichangamkia hii fursa kwa kujiunga nasi na kufurahia kwa pamoja mchezo wa soka kupitia visimbuzi vyetu,” alihitimisha Hanif.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...