NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura amewataka vijna kutumia fursa ya Tamasha la Kimataifa la 35 la Sanaa na Utmaduni Bagamoyo kuonesha vipaji kwa ajili ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi.
Akifungua Tamasha hilo juzi ambalo mwaka huu limeshirikisha vikundi 65 vya sanaa na utamaduni kutoka nchini na nje ya nchi, Naibu Waziri huyo alisema sanaa ni ajira yenye uhakika kama wasanii watafanya kazi zao kwa uadilifu.
Mhe. Wambura amesema anafahamu changamoto zinazoikabili Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa za ukosefu wa fedha  na wafadhili hivyo aliwataka kushirikisha wadau wa ndani na nje ili matamasha kama hayo yaboreshwe na kushirikisha nchi mbalimbali duniani.
Alisema kutoka TaSUBa kianzishwe mwaka 1982 kimekuwa kivutio na kubadilishana tamaduni na nchi mbalimbali kama Ujerumani, Norway, Kenya, Japan na China ambazo zimeshiriki kwaka huu katika tamasha hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa wa wizara hiyo, Francis Songoro aliwaomba wadau waendelee kujitokeza kuwatia moyo wasanii katika kazi zao.
Katika tamasha hilo Naibu Waziri aliongoza kucheza ngoma ya Kigogo huku kikundi cha wanachuo kikitia fora kwa ngoma ya asili ya Kizaramo kutoka mkoa wa Pwani ya Mkwaju Ngoma.
Awali Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majjid Mwanga aliwataka wananchi wa Bagamoyo kukienzi chuo hicho ambacho ni cha kwanza Tanzania kinachozalisha wasanii nchini na kukuza uchumi wa wilaya kwa kuwapokea wageni wengi wanaokuja kujifunza sanaa ya Tanzania.
Tamasha la TaSUBA litafanyika kwa wiki mmoja mfululizo ambako vikundi mbalimbali vitaonesha umahiri wao wa kucheza, kuimba na bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kutumia vifaa vya asili.
Pia katika tamasha hilo ambalo Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) iliwakilishwa na wajumbe sita wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa mtadano huo Suleiman Kissoky ambako kikundi chao cha ngoma na sarakasi cha Splendid kitawakilisha.
 Wapiga ngoma wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) wakipiga ngoma katika ufunguzi wa tamasha hilo. 
 Wacheza ngoma za utamaduni wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) wakitumbuiza katika ufunguzi wa tamasha hilo. 
 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo, Anna Wambura (katikati)akifuatilia ngoma ya kikundi cha wanachuo wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBA) wakicheza ngoma ya Kizaramo ya Mkwaju Ngoma kutoka mkoa wa Pwani. Kushoto ni Dkt. Herbert F. Makoye Mkurugenzi Mtendaji wa TaSUBa na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majjid Mwanga.
 Wadau mbalimbali wa sanaa kutoka sehemu mbalimbali wakifuatilia maoneshoa ya ngoma wakati wa ufunguzi
 Wadau wa sanaa  wakifuatilia maoneshoa ya ngoma wakati wa ufunguzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...