Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba akiongea na Vyombo vya Habari juu ya hatua za Serikali za kuzuia utupaji ovyo wa taka hatarishi za Hospitalini na  kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ifikapo Januari mosi 2017. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bw. Richard Muyungi.
­­­­


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
tz
TANGAZO KWA UMMA

UZUIAJI WA UTUPAJI OVYO   USIO WA KITAALAMU WA TAKA ZA MAHOSPITALI. 

Sheria ya usimamizi  wa Mazingira ya mwaka 2004  inapiga marufuku uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na unaotokana na taka za mahospitali.  Aidha Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009, zinasisitiza utenganishi wa taka mbali mbali  zitokazo kwenye mahispotitali kwa kuzitibu katika namna ambayo haitaleta athari katika mazingira na afya ya binadamu. Pia Kanuni zinahimiza matumizi ya teknologia sahihi kama vile matumizi ya incinerators ambazo huchoma taka za mahospitali na  kuziteketeza kabisa.

Ofisi yangu imefuatilia na kugundua kuwa taka nyingi za mahopitali, taka kutoka katika maduka ya  madawa zilizoisha muda wake zinatupwa ovyo  au kuharibiwa kwa utaratibu usio kubalika kitalaamu. Tumefuatalia na kukuta malundo ya madawa chakavu na vifaa vya hospitali vilivyotumika   katika maeneo ya visiwa vya Bongoyo na Mbudya. Aidha madawa chakavu yanatumpwa holela katika dampo la Pungu Kinyamwezi.  Hii ni hatari sana kwa mazingira na kwa afya ya binadamu.

Kuanzia sasa ni marufuku  kutupa taka hizi katika utaratibu usio wa kawaida. Kila hospitali na zahanati  au kituo cha afya kihahakikishe kinatumia incinerators  au utaratibu mwingine ulio sahihi kwa mujibu wa sheria ya mazingira na kanuni zake. Aidha ninaiagiza NEMC kuanzia sasa wafanye msako mkali kubaini mahospitali na watu wanaokiuka agizo hili. Nimewapa mwezi mmoja na   kwa  wale wanaofanya hivyo waache mara moja.   Kwa msako huu atakayebainika kukiuka hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi yake.Nichukue fursa hii kutoa tena pole kwa wezentu wa Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani kwa athari za tetemeko la ardhi.

Baada ya tatetemeko kuna athari kubwa za kimazingira  ambazo zimejitokeza. Hivyo mimi binafsi ninafuatilia suala hili kwa ukaribu na kuhakikisha  athari ambazo zimejotokeza na zinazoendelea kujitokeza zinashughulikiwa kwa haraka.  Nimeagiza Ofisi yangu pamoja na NEMC washirikiane kwa ukaribu sana na watendaji wa Mkoa na Kamati mbalimbali zilizoundwa kushughulikia maafa haya na kufanya  tathmini  ya athari za mazingira zilizojitokeza na kuelekeza hatua za haraka kuchukuliwa ilikupunguza madhara kwa mazingira na binadamu.

Pia, napenda kutumia fursa hii  kuukumbusha umma  juu ya dhamira ya Serikali ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko na vifungashio vya ya plastiki ifikapo Januari Mosi 2017.Adhma ya Serikali ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko  na vifungashio vya plastiki ni kuepusha athari za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na matumizi ya mifuko hiyo. Hivyo basi wazalishaji, waagizaji, wasambazaji, wauzaji  na watumiaji  wa mifuko hiyo wanakumbushwa kuendelea na zoezi la kuondosha pamoja na kusitisha uzalishaji wa mifuko hii.

IMETOLEWA NA
JANUARY  Y. MAKAMBA (MB.)
WAZIRI WA NCHI OFISI YAMAKAMU WA RAIS
MUUNGANO NA MAZINGIRA

21/9/2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...