SHIRIKA
la Umeme Tanzania ( TANESCO) linapenda kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa leo Jumamosi tarehe 24/09/2016 kumetokea hitilafu
katika Kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza Umeme cha Ubungo 220kV/
132kV na kusababisha kukosekana Umeme kwenye maeneo ya jiji la Dar es
Salaam yanayotegemea Vituo vya Kunduchi na Makumbusho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu jijini mapema leo, tayari hatua za kurekebisha hitilafu hiyo zinaendelea kuchukuliwa ambapo mafundi wa TANESCO wanaendelea na kazi ya kurekebisha hitilafu hiyo na umeme utarejea masaa machache yajayo.

Taarifa
hiyo inawaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu wowote utakaojitokeza.
hili shirika livunjwe. ni kubwa sana kuwa moja. zitengenezwe kampuni mbili zinazoshughulikia uzalishaji na nyingine usambazaji
ReplyDelete