Serikali ya Tanzania na Iran zakubaliana kuanzishwa kwa wiki ya Utamaduni itakayowezesha kujifunza namna ya kuukuza ,kuulinda na kuendeleza sekta hiyo.

Makubaliano hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokutana na Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran (kushoto) Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Tanzania na Iran.

Waziri Nnauye alisema kuwa amekubaliana na wazo la kuanzishwa kwa wiki ya Utamaduni kati ya Tanzania na Iran na ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwao namna ya kuukuza, kuulinda na kuuendeleza utamaduni wa mtanzania.

“Utamaduni ni silaha ya upendo na nimefurahia wazo la kuanzisha wiki ya Utamaduni na tuko tayari kujifunza kutoka kwenu na hakika tumelipokea na tunaamini fursa hii italeta mafanikio makubwa katika sekta hii”, alisema Mhe. Nnauye.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Utamaduni Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman aliihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa wataendelea kushirikiana katika masuala ya Utamaduni na kuendelea kujifunza kutoka kwa watanzania namna bora ya kuenzi,kuendeleza na kuutunza Utamaduni.

Naibu Waziri huyo wa Iran aliendelea kusema serikali yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika uandaaji wa Filamu na kubadilishana uzoefu katika masuala ya filamu kati ya nchi hizo mbili.

Hata hivyo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nnauye alipata mwaliko kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni Iran Mhe. Turkaman kwenda nchini Iran kujionea vivutio vya utamaduni.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran (wa tatu kushoto) Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam walipokutana kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2, 2016 wa pili kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai na kushoto ni Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Iran Bw. Ali Bagiri. 
Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran (wa tatu kushoto) Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman akielezea azma yake ya kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Utamaduni kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Septemba 2,2016 wa pili kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai na kushoto ni Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Iran Bw. Ali Bagiri.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman (katikati) walipokutana Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2,2016 kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea zawadi ya kiutamaduni kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman (katikati) walipokutana Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2, 2016 wa kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akiangalia kitabu cha Utamaduni kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman (katikati) walipokutana Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2, 2016 wa kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai. 
Picha/Habari na Raymond Mushumbusi .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...