Arusha. Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) zimetwaa ubingwa wa bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha.

Taswa FC na Taswa Queens ambazo zinadhaminiwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia na Benki ya Posta Tanzania (TPB) zilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika bonanza hilo la kusisimua na waandishi kushindana katika michezo mbalimbali mbali ya soka na netiboli.

Timu ya Wazee Club ambao ilishika nafasi ya pili, ndiyo pekee iliyonusurika na kichapo katika bonanza hilo aada ya kuambulia sare ya mabao 2-2. Hata hivyo, timu hiyo ilibidi ifanya kazi ya ziada baada ya kusawazisha mabao mawili katika dakika sita za mwisho. Timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji cha AJTC kilishika nafasi ya tatu na timu ya mwisho ni Redio Sunrise.

aswa FC ilianza kwa kasi na kufunga mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa Saidi Seifu akipokea pasi safi za Majuto “Dr Regret” Omary. Martin Shila, Edrward Mbaga, Muhidin Sufiani, Zahoro Mlanzi, Salum Jaba na kipa wao, Mwarami Seifu walikuwa kizingiti kikubwa katika mechi zote.

Katika mechi ya pili, Taswa FC ilishinda mabao 4-0n dhidi ya Sunriseb Redio , bao la kwanza likifungwa na kapteni, Wilbert Molandi kwa kuunganisha kona ya Hare Temba na baadaye Saidi Seifu akifunga mabao matatu kufutia pasi ya Athumani Jabir na Majuto Omary ambaye alitoa pasi ya bao la tatu na la nne.

Katika mchezo wa mwisho, Taswa FC iliibuka na ushindi wa ba 1-0 dhidi ya AJTC, bao la dakika za majeruhi lilifungwa na Ali “Maradona” Salum kufuatia kona safi ya Majuto.Timu ya netiboli ya Taswa Queens ilifanya ‘mauaji’ kufuatia ushindi wa mabao 30-2 dhidi ya AJTC. Mabao ya Taswa Queens yalifungwa na Sharifa Mustapha aliyefunga mabao 22 na Rose Michael aliyefunga mabao nane.

Taswa Queens ilitawala sana mchezo huo kupitiaa wachezajia wake, Zuhura Abdinoor, Johari William, Elizabeth Mbasa, Tatu, Mage na Vicky Godfrey.
Timu zote hizo zilizawadiwa kitita cha sh 100,000 kila moja na kombe. Kwa upande wa kukimbiza Kuku, Taswa Queens pia walifanikiwa kuibuka na ushindi wakifuatiwa na Sunrise Radio ambao wote waliondoka na kuku kila mmoja.

Mgeni rasmi katika bonanza hilo la 11 lillilofanyika katika viwanja vya General Tyre alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro ambaye alisema kuwa waandishi wa habari ni muhimu kushiriki michezo ya aina mbalimbali ili kuiweka miili vizuri.

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Bonanza la 11 nahodha wa timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini(Taswa FC),Wilbert Molandi katika fainali la Bonanza la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha kwenye uwanja wa General Tyre jumapili,kulia ni Mwenyekiti wa Taswa FC,Majuto Omary na kushoto ni Mratibu wa mashindano hayo,Mussa Juma.

Nahodha wa timu ya Netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC)Zuhura Abdulnoor na mchezaji mkongwe wa Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini,(Taswa FC),Muhidin Sufiani(kulia)wakifurahia ushindi.

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akizungumza katika Bonanza la 11 la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha.  
Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na waratibu wa bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...