Na Mwandishi Maalum, New York

Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali, kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa takribani wiki nzima iliyopita wameendelea kuelezea vipaumbele vya nchi zao mbele ya wajumbe wanaohudhuria Baraza Kuu la 71 la UMoja wa Mataifa.

Mambo makubwa ambayo karibu kila kiongozi ameyagusia katika hotuba yake ni pamoja na tatizo la kuongezeka kwa matukio ya ugaidi, tatizo la wakimbizi na wahamiaji, vita na machafuko vinavyoendelea katika nchi kadhaa, ubaguzi kwa misingi ya dini au eneo analotoka mtu, mabadiliko ya tabia nchi na utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo endelevu.

Pamoja na viongozi hao kushiriki katika majadiliano ya jumla ya Baraza Kuu, lakini pia wamekuwa wakishiriki mikutano mingine ya pembezeni ambayo imeandaliwa sambamba na mkutano mkuu.

Aidha mikutano ya kimataifa na mikubwa kama huu wa 71 wa Baraza Kuu pia hutumika na viongozi wakuu na wa nchi na serikali kama sehemu ya kukutana na kufanya mazungumzo na kuweka mikakati ya mahusiano baina ya nchi zao.

Kama ilivyokuwa kwa Viongozi wengine, kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Dkt.Augustine Mahiga ( Mb) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pia ametumia fursa ya mkutano huu kukutana na viongozi wengine na kubadiliana mawazo na kujadiliana miongoni mwao mambo kadha wa kadhaa yenye maslahi kwa pande zote mbili.

Yafuatayo ni baadhi ya matukio ambayo Mhe. Waziri Mahiga ameshiriki nje ya majadiliano ya Jumla. Leo Jumatatu Waziri atapata fursa ya kuelezea vipa umbele vya Tanzania wakati atakaposoma hotuba yake.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika Mkutano wa Mawaziri wa Nje wa nchi za Jumuiya ya Madola.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga alipoongoza kikao cha Troika ya SADC.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akibadilishana mawazo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sultanate of Oman, Bw. Yusuf bin Alawi bin Abdullah.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika Mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwaiti, Bw Sabah Al KHalid Ala Sabah
Diplomasia ya Corridon, Hapa Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, akiwa na ujumbe wa Morocco.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Belgium Bw. Alexander De Croo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...