THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Waziri Mahiga aongoza Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya SADC Uchaguzi wa Jamhuri ya Shelisheli

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb.), jana tarehe 2 Septemba, amezindua Misheni ya Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC kwenye uchaguzi wa Jamhuri ya Shelisheli kwa niaba ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika -SADC Organ. 
Misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi itakayojumuisha waangalizi kutoka nchi za SADC, itashiriki kwenye uangalizi katika vituo vyote 25 vya upigaji kura nchini Shelisheli. 
Pamoja na kuongoza misheni hiyo, Tanzania kama Mwenyekiti wa SADC Organ itaongoza timu za uandishi wa taarifa ya SADC pamoja na ufuatiliaji wa taarifa za vyombo vya habari kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi nchini humo unaotarajiwa kufanyika tarehe 8-10 Septemba, 2016. 
Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza asasi hii muhimu ya Jumuiya, wakati wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016. 
Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mhe. Dkt. Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kumwakilisha Mhe. Dkt. Magufuli, katika kuongoza ujumbe wa Waangalizi wa SADC. 
Wajibu wa Tanzania kuongoza Misheni hya Waangalizi wa Uchaguzi imetokana na misingi na muongozo wa Jumuiya ya SADC ya kuwa na chaguzi za kidemokrasia katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika. Waziri Mahiga anatarajiwa kutoa taarifa ya awali ya Misheni hiyo ya waangalizi wa SADC Septemba 12, 2016. Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustino Mahiga akifungua Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge tarehe 2 Septemba, 2016, Mahe Seychelles. Mhe Waziri anamuawakilisha Mhe. Rais John pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na  Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge tarehe 2 Septemba, 2016 huko Mahe, Seychelles.