Na Daudi Manongi,MAELEZO

KAMISHENI ya mchezo wa ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) imevitaka vikundi na asasi zinazojishughulisha na usimamizi na utaribu wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini kuacha mara moja kwani ni kinyume na sheria,kanuni na taratibu za mchezo huo.

Hayo yamesemwa leo na Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) Bw.Chaurembo Palasa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

“Kumekuwa na vyama, asasi na vikundi ambavyo vimesajiliwa Brela lakini havikufata taratibu za sheria wala hawana vibali vya kuendesha mchezo wa ngumi nchini kutoka kwetu, tunawataka kuacha mara moja kwani ni kuvunja sheria”.

Aidha Chaulembo alisema vyama hivyo kuwa ni hewa kwani hakuna sheria, kanuni za mchezo huo za mwaka 1967, 1971 na 1999 zinazowatambua kuwa ni wasimamizi na waratibu mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.

Kwa upande wake Katibu msaidizi wa kamisheni hiyo Bw.Chatta Michael amewataka wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini kuwa na leseni na vibali toka katika kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini ambapo alitaja tarehe ya mwisho kutoa vibali hivyo ni Octoba 19 mwaka huu.

Aidha Chatta aliwataka waandaaji wa mapambano ya ngumi za kulipwa kuomba vibali vya uandaaji wa mapambano hayo angalau siku kumi na nne(14) kabla ya pambano.

Akifafanua zaidi alisema waandaaji hao pia wanatakiwa kubainisha maeneo watakayotumia,uzito wa bondia, mkanda unaoshindaniwa,utaifa wa bondia,wasimamizi wa mchezo na malipo kwa mabondia husika.

Aliongeza kuwa kamisheni inatoa pongezi kwa wadau wote wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini wakiwemo mabondia, waamuzi, makocha, wakufunzi, viongozi wa makampuni na taasisi zinazojiusisha na mchezo wa ngumi za kulipwa nchini kwa kuendeleza mchezo huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...