THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TPDC YAWASHIKA MKONO WANA-KAGERA

Kufuatia hali inayoukabili mkoa wa Kagera kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo mnamo septemba 10 mwaka huu na kusababisha maafa makubwa kwa baadhi ya Wananchi na hata kuchukua uhai wa watu 17 Mkoani humo
Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) limeungana na jitihada za Serikali katika kusadia waathirika wa tetemeko Mkoani humo kwa kutoa  vifaa vya ujenzi ikiwa ni pamoja na saruji na mabati vyenye thamani ya shilingi millioni 20 kwa ajili ya kusaidia ujenzi kwa walioguswa na maafa hayo.
Baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TPDC Mhandisi, Kapuulya Musomba amesema kuwa wametoa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi millioni 20 kwa ajili ya kuwasadia waathirika wa tetemeko hilo.
Pia Mhandisi Musomba amesema kuwa misaada waliotoa sio mwisho badala yake watahakikisha wanaendelea kuwafuatilia kampuni washirika wanaofanya kazi na TPDC nchini, huku akiongeza kuwa tayari wameshawaandikia barua ya kuwaomba kuchangia na kushiriki katika kusaidia Wanakagera.
 Kaimu Mkurugenzi wa TPDC Mhandisi, Kapuulya Musomba akipeana  mikono na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni ishirini (20,000,000) kwa waathirika wa tetemeko Mkoani Kagera.
 Mjumbe wa Bodi ya TPDC Balozi Ben Moses akikabidhi nyaraka zenye orodha ya vifaa vya ujenzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu vilivyo kabidhiwa na TPDC.
Zoezi la kukabidhi misaada iliyotolewa na TPDC kwa waathirika watetemeko Mkoani Kagera likiendelea.