Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer akizungumza na wadau wa habari kwenye maadhimisho Siku ya Kimataifa ya Haki za Kupata Taarifa Septemba 28 KATIKA ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wameibuka washindi wa TUZO ya UFUNGUO WA DHAHABU kwa kuwa taasisi inayofunguka zaidi kwa wananchi hapa Tanzania kwa mwaka 2016. Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika katika hoteli yaa Sea Shells hapa Dar es Salaam.
Katika tuzo hizo Wizara ya Sheria na Katiba imeambulia Kufuli la Dhahabu kwa kuwa taasisi ngumu kwa upatikanaji wa taarifa kwa Umma.
MISA Tanzania pia walizindua Ripoti ya kila mwaka ya Upatikanaji Taarifa katika Taasisi za Umma kwa mwaka 2016.

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer akiwazungumza jambo na Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa baada ta tuzo ya Kufuli la Dhahabu kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2016 lililokwenda kwenye Wizara ya Sheria na Katiba
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Makao, Gabriel Mwangosi baada ya kutwa tuzo ya TRA katika utoaji wa taarifa kwa umma. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...