NAULI ya abiria wa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu jijini Dar es Salaam, imepanda kutoka Sh 400 ya awali hadi 600.
Tozo hiyo ya nauli mpya inatarajiwa kuanza rasmi Septemba mosi, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Ng’hwani Kudema, alisema viwango hivyo vya nauli vilivyokokotolewa na Mamlaka ya Majini na Nchi Kavu (Sumatra), vimepanda kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu.
“Baada ya siku 14 nauli hizi zitaanza kutozwa kwa mujibu wa utaratibu na hili tutabandika matangazo. 
Hadi kufikia Septemba 13, mwaka huu nauli itakayokuwa inatozwa ni shilingi 600 kwa mtu mzima na shilingi 100 kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,” alisema Kudema
Alisema wakati wa majaribio ya treni hiyo Agosti mosi mwaka huu, walikuwa na mabehewa 10 lakini kutokana na mahitaji ya usafiri huo kuwa mkubwa, walilazimika kuongeza mabehewa ambayo kwa sasa yamefika 18.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...