Na Daudi Manongi,MAELEZO


Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) imejitolea kudhamini pambano la kuchangia waathiriwa na tetemeko la Ardhi Kagera litakalofanyika siku ya Jumapili saa tisa kamili kati ya Wasanii wa Bongo Movie na Bongo Fleva katika uwanja wa Taifa.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Biashara wa kampuni hiyo Bw.Jahu Mohamed Kessy wakati akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

“Sisi kama Tanzania Sisi Nyumbani(TSN) tumejitolea kudhamini pambano hili kwa kushirikiana na wasanii hawa kwa kuwa tumeguswa na janga hili na hivyo mbali na michango mbalimbali tukaona ni vyema tujitolee kuwapa Mipila na Jezi kwa wasanii hawa ili kuhamasisha uchangiaji huu ”Aliongeza Bw.Kessy.

Aidha Bwana Kessy alisema kuwa wao kama TSN wanaunganisha nguvu ya wasanii hawa kutoka katika tasnia hizi mbili tofauti, kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji huu kwa pamoja.

Pia amewataka wananchi,mashirika na makampuni mengine binafsi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchangia na kuwezesha misaada kwa wananchi wa kagera waliopata maafa kutokana na tetemeko hilo la Ardhi.

Kwa upande wake mwakilishi wa Bongo Movie Bw.Steve Nyerere amesema kwamba wao kama bongo movie wameguswa na jambo hili na ndio maana wamejitokeza kutumia vipaji vyao ili kile kitakachopatikana ili kiweze kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi Kagera.
 Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, wakati akikabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera. Kushoto ni Kapteni wa Timu ya Bongo Movie Jimmy Mafufu.
 Mwakilishi wa Timu ya Bongo Fleva, Kalapina (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, wakati makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera. Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy na Mwakilishi wa Bongo Movie Steve Nyerere.
 Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Bongo Movie Jimmy Mafufu, wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera. Kulia ni mwakilishi wa Bongo Movie Steve Nyerere.
 Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Bongo Fleva M2 the P, wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akiwakabidhi vifaa vya michezo wawakilishi wa Bongo Movie na Bongo Fleva  kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Picha na Frank Shija, MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...