Na Zuena Msuya, Tunduru ,RUVUMA, 

Wizara ya Nishati na Madini, kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini(SMMRP) imepokea jengo la ofisi ya Madini Mkazi wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma kutoka kwa kampuni ya ukandarasi ya Mkongo Contractors ili kuanza kutumika na ofisi hiyo baada ya kufanyiwa ukarabati .

Akizungumza mara baada ya kupokea jengo hilo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma hivi karibuni, Msanifu Majengo wa SMMRP , Joseph Ringo alisema kuwa lengo la kufanya ukarabati katika jengo hilo ni kuimarisha shughuli za kiutendaji katika uendelezaji wa shughuli za madini wilayani ya Tunduru na viunga vyake ukizingatia kuwa wilaya hiyo imejikita zaidi katika uchimbaji wa madini ya vito vya aina mbalimbali.

Aidha Msanifu majengo Ringo Alifafanua kuwa kama ilivyo dhamira ya mradi wa SMMRP ,kufanyika kwa ukarabati katika jengo hilo kutawezesha Afisa Madini Mkazi wa eneo hilo kufanya kazi zake kwa ufanisi na kufikia malengo aliojiwekea katika kuwahudumia wadau wa madini.

Vilevile alisema kuwa ukarabati wa jengo hilo umefadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ambao umejumuisha vifaa vya kisasa ikiwemo kuunganishwa na mfumo mpya na wa kisasa wa TEHAMA ambao unarahisisha utunzani wa kumbukumbu za wadau wa madini tofauti na ilivyokuwa hapo awali. 

Kwa upande wake Ofisa Madini mkazi Tunduru, Mhandisi Fredrick Mwanjisi aliupongeza mradi wa SMMRP kwa kuboresha na kuzijengea uwezo ofisi za madini nchini ili kuboresha shughuli za uendelezaji wa rasilimali za madini.

Hata hivyo Mhandisi Mwanjisi ameushauri mradi wa SMMRP,kutumia muda mfupi katika kutekeleza shughuli zake za ukarabati na ujenzi wa majengo mbalimbali kwa lengo la kuendeleza rasilimali madini.

Naye Mkurugenzi Msaidizi rasilimali watu wa Wizara ya Nishati na Madini,Joyceline Lugora, amewataka maafisa madini wakazi na wakanda zote nchini kutunza miundombinu ya majengo hayo ili kuondoa gharama za ukarabati wa mara kwa mara.

Na pia ichukue muda mfupi kukarabati eneo lililoharibika endapo kumetokea uharibufu katika jengo



Taswira tofauti za muonekano wa jengo la Ofisi ya Madini Mkazi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, jengo hilo limejengwa na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini ( SMMRP) unaotekelezwa na Benki ya Dunia.

Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini,Wasanifu majengo pamoja na Wakandarasi waliojenga jengo la ofisi ya madini Mkazi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakifanya ukaguzi wa jengo hilo kabla ya kukabidhiana ili lianze kutumiwa na Ofisi ya Madini Tunduru, jengo hilo litazinduliwa rasmi hivi karibuni. 
Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini,Wasanifu majengo pamoja na Wakandarasi waliojenga jengo la ofisi ya madini Mkazi wilani Tunduru mkoani Ruvuma wakifanya ukaguzi wa jengo hilo kabla ya kukabidhiana ili lianze kutumiwa na Ofisi ya Madini Tunduru, jengo hilo litazinduliwa rasmi hivi karibuni. 
Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali watu wa Wizara ya Nishati na Madini Joyceline Lugora ( mstari wa mbele wa pili kushoto) akikabidhi ufunguo wa jengo la ofisi ya Madini Mkazi Wilani Tunduru mkoani Ruvuma, kwa Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Nyasa, Mhandisi Fred Mahobe,( mstari wa mbele wa pili kulia) mara baada ya kukabidhiwa kutoka kiongozi wa timu ya ushauri ya ujenzi wa jengo hilo, Msanifu Majengo Paul Mshana (kushoto katikati) aliyepewa dhamana ya kusimamia ujenzi wa jengo hilo. 


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...