THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TUTAPITIA UPYA SABABU ZA KUANZISHWA KWA RUBADA - MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itapitia upya sababu za kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) kufuatia mamlaka hiyo kuendeshwa kwa ubabaishaji.

Hatua hiyo imekuja baada ya mamlaka hiyo kushindwa kusimamia uendelezaji wa bonde hilo na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ikwiriri mkoani Pwani.

Alisema baada ya mapitio hayo shughuli za mamlaka hiyo zitahamishiwa kwenye mamlaka nyingine za serikali kwani RUBADA  imeshindwa kufanyakazi hiyo kwa muda mrefu.

“RUBADA wamepewa ardhi lakini wameshindwa kuiendeleza, tutafanya upya mapitio ya kuanzishwa kwake,” alisema.
Akizungumzia kuhusu Kampuni ya Agro Forestry Plantation inayotaka kujenga kiwanda cha sukari wiyani Rufiji aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha asilimia 60 ya watumishi watakaowaajiri wawe ni vijana wa wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, kwenda wilayani Rufiji kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya ya Mkuranga na Ikwiriri.

Waziri Mkuu amelitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Ikwiriri kuhusu kutotatuliwa kwa mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu.

Naye Mkurugenzi wa halshauri ya wilaya hiyo, Rashidi Salum alimweleza Waziri Mkuu kuwa, mgogoro huo umeshatatuliwa kwa ngazi ya wilaya  hivyo hatua iliyosalia ni kwa uWaziri wa Ardhi kufika na ramani ili kutoa uamuzi.