Serikali ya Uingereza inatarajia kutoa takribani TZS 6.3 bilioni (sawa na Paundi 2.23
milioni) kusaidia ukarabati wa shule baada ya athari za tetemeko la ardhi mkoani
Kagera mnamo Septemba 10.
Msaada huu wa ziada umetangazwa mapema leo wakati Balozi mpya wa Uingereza
nchini Tanzania, Sarah Cooke alipokuwa akikabidhi hati ya kibalozi kwa Mheshimiwa
Rais wa Magufuli.
Hii ikifuatiwa na ziara iliyofanywa na Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiambatana na Mkuu wa Idara ya Kimataifa
ya Maendeleo ya Uingereza (DFID), Ndugu Vel Gnanendran.
Misaada hii itatumika katika kukarabati, kuboresha na kuwezesha Shule ya
Sekondari ya Ihungo kuwawezesha zaidi ya wanafunzi 740 kuendelea na masomo
yao mapema iwezekanavyo. Kwa kuongezea, Serikali ya Uingereza itasaidia pia
kukarabati nyumba za walimu katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya
Rugambwa ambazo zilianguka. Shule hizi ndizo ambazo zimeathiriwa zaidi katika
tetemeko la ardhi.
Balozi Mpya, Sarah Cooke alisema; “Serikali ya Uingereza inapenda kutoa salamu
zake za masikitiko kwa wale wote ambao wameathirika na tetemeko la ardhi Kagera.
Tunaona ni muhimu sana kusaidia Wizara ya Elimu mapema iwezekanavyo ili
kuwawezesha watoto wa Bukoba wasiendelee kuangaika zaidi na kuweza
kuendelea na masomo yao ndani ya muda mfupi iwezekanavyo.
Hivyo basi,
tunapenda kutangaza rasmi kwamba Uingereza itatoa msaada wa ziada kusaidia
elimu iendelee kutolewa hasa katika kipindi hiki cha athari za tetemeko Bukoba”
Serikali ya Uingereza itadumu imara katika kutoa ushirikiano kwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania katika jitihada zake za kuboresha elimu kwa watoto wote
wa Tanzania.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupoka msaada wa Shilingi Bilioni 6.3 kutoka Idara ya Maendeleo ya Nje ya nchini Uingereza (DFID) ikiwa ni sehemu ya kusaidia Shule zilizoathirika na tetemeko la Ardhi mkoani Kagera leo jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mkuu wa Idara ya DFID hapa nchini, Vel Gnanendran.
Mkuu wa Idara ya DFID hapa nchini, Vel Gnanendran akizungumza na waandishi wa habari juu ya Serikali ya Uingereza kutoa msaada wa Shilingi Bilioni 6.3 wenye lengo la kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi hususan kwa shule zilizoathiriwa na tetemeko hilo. kulia ni Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Profesa Joyce Ndalichako. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...