THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

UJUE UWANJA WA AMAAN, ZANZIBAR

Uwanja wa Amaan mjiniUnguja ni wa kihistoria, japo wengi hawafahamu. Ulijengwa kwa msaada wa serikali ya China na ulifuynguliwa mwaka 1970, ukiwa ni mradi mkubwa wa nchi hiyo wa viwanja vya michezo barani Afrika. Michezo na sherehe nyingi hufanyika uwanjani hapo. Sherehe kubwa ya kihistoria ilifanyika February 5, 1977 wakati vyama vya TANU na Afro Shirazi vilipoungana na kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM.  Uwanja huo ulifungwa kwa muda na kufanyiwa ukarabati mkubwa kabla ya kufunguliwa tena mwaka 2010. Una uwezo wa kukaa watu 15,000. 
Pia ni uwanja wa kwanza kuweza kuchezewa mechi usiku hapa nchini.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. HK Anasema:

    Kwa nyogeza tu pia uwanja huu wa Amani ndio uwanja wa mwanzo na wa pekee Tanzania (Sina hakika kwa Afrika kwa wakati huo) ila ndio uliokuwa ukicheza baadhi ya mechi zake hata wakati wa Usiku. Kwa kweli una historia katika nchi yetu.