Uwanja wa Amaan mjiniUnguja ni wa kihistoria, japo wengi hawafahamu. Ulijengwa kwa msaada wa serikali ya China na ulifuynguliwa mwaka 1970, ukiwa ni mradi mkubwa wa nchi hiyo wa viwanja vya michezo barani Afrika. Michezo na sherehe nyingi hufanyika uwanjani hapo. Sherehe kubwa ya kihistoria ilifanyika February 5, 1977 wakati vyama vya TANU na Afro Shirazi vilipoungana na kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM.  Uwanja huo ulifungwa kwa muda na kufanyiwa ukarabati mkubwa kabla ya kufunguliwa tena mwaka 2010. Una uwezo wa kukaa watu 15,000. 
Pia ni uwanja wa kwanza kuweza kuchezewa mechi usiku hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwa nyogeza tu pia uwanja huu wa Amani ndio uwanja wa mwanzo na wa pekee Tanzania (Sina hakika kwa Afrika kwa wakati huo) ila ndio uliokuwa ukicheza baadhi ya mechi zake hata wakati wa Usiku. Kwa kweli una historia katika nchi yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...