THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

UKAWA YASITISHA TENA MAANDAMANO YA UKUTA


Mwenyekiti  wa Chama cha CHADEMA Taifa Mhe. Freeman Mbowe


Na Anthony John,
Globu ya Jamii
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  kimesitisha  shughuli  zote  za maandamano na mikutano nchi nzima,kwa kudai kuwa ukuta ni fikra endelevu na si mpango wa siku moja.
 Hayo yamesemwa leo na  Mwenyekiti  wa Chama hicho Taifa,Mh.Freeman Mbowe wakati  akizungumza  na Waandishi  wa Habari,Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.
Mbowe amesema kuwa wataendelea Kujipanga katika kulinda  Haki yao ya kidemokrasia kama ambavyo katiba ya vyama vya siasa inavyosema,kuwa ni haki yao ya kidemokrasia.
‘’Mapambano  ya  kisiasa si tukio la siku moja ni tukio endelevu na kwa hiyo tarehi Mossi ,Oktoba ambayo ilikuwa ni siku mbadala ya maandamano maalum,hivyo kwa niaba ya kamati kuu imeona kuna umuhimu  wa kusimamisha maandamano maalumu na mikutano nchi nzima ilikupisha mbinu nyingine mbalimbali’’amesema Mbowe


Kuna Maoni 4 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Njaa zinasumbua sana vichwa vya watu. Angalau leo umempa sekunde 20.

 2. Anonymous Anasema:

  Hizo njaa zisituchafulie nchi basi. hawa jamaa wa kusini wana agenda nyingine. Mbona Moshi mjini kutulivu na hawafanyi fujo huko?

 3. Anonymous Anasema:

  hakuna maandamano. Mnatishia nyau tingatinga?? Acheni kuwaongepea wananchi hakuna cha maandamano.

 4. gassim Anasema:

  Mbona magazeti ya Tanzania yanapenda uchochezi baina ya serikali Na upinzani baada ya kuandika maneno ya kuwapongeza wanatia vitina sio sawa