Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wameendelea kuwa miongoni mwa wananchi walioanza kuchukua
Vitambulisho vipya vya Taifa vyenye saini; kufuatia utaratibu uliotangazwa hivi
karibuni na Nida wa kuanza kugawa vitambulisho vipya kwa makundi mbalimbali
waliokamilisha taratibu za usajili.
Shughuli ya
kugawa Vitambulisho vya Taifa kwa Waheshimiwa Wabunge zimeendelea katika siku
ya pili bungeni Dodoma; pamoja na kuwasajili wabunge ambao kwa sababu moja au
nyingine hawakusajiliwa wakati wa zoezi la awali la usajili.
Mbali na
waheshimiwa Wabunge; wengine ni wafanyakazi wa Bunge na watumishi katika
taasisi na Wizara mbalimbali ambao walisajiliwa katika utaratibu wa kawaida wa
Usajili. Zaidi ya waheshimiwa Wabunge 240 watapatiwa vitambulisho vyao.
Zoezi la
ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa linaendelea katika ofisi zote za usajili za
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kwa wale wananchi ambao hawakuwahi kupata
vitambulisho awali. Kwasasa hakutakuwa na kubadilisha vitambulisho vya zamani
kwa wale waliokwisha pata awali kwani Vitambulisho vya zamani vitaendelea
kutumika sambamba na vipya katika matumizi mbalimbali yaliyokusudiwa
Waziri
wa Nishati na Madini na Mbunge wa jimbo la Musoma, Mhe.Profesa Sospeter Muhongo
akipokea Kitembulisho chake cha Taifa chenye saini kwa furaha kubwa kutoka kwa
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Na Hifadhi Hati NIDA. Bi. Rose Mdami
Mheshimiwa
Waziri wa Katiba na na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe, akiwa mwenye furaha kubwa
baada ya kuchukua Kitambulisho chake kipya Bungeni Dodoma. NIDA imeanza kutoa
vitambulisho vipya vyenye saini kwa viongozi wakiwemo Waheshimiwa Wabunge zoezi
linaloedelea mkoani Dodoma sambamba na kikao cha Bunge.
Mheshimiwa
Deo Sanga, akieleza faida ambazo tayari ameshazipata kwa kutumia Kitambulisho
chake cha Taifa. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi
hati NIDA Bi, Rose Mdami. Mhe. Sanga amepokea kitambulisho chake leo katika
Ofisi za Bunge Dodoma
Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipata huduma kutoka kwa maafisa
wa NIDA ambao wapo bungeni hapo kutoa vitambulisho vipya kwa waheshimiwa
wabunge Mjini Dodoma.
Mbunge
wa Muheza na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Bunge Mheshimiwa
Adadi Rajabu akipokea kitambulisho chake kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Hifadhi Hati NIDA Bi. Rose Mdami katika Ofisi za Bunge Mjini
Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...