THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

VODACOM YAENDELEA KUFANIKISHA WIKI YA USALAMA BARABARANI.

  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamanda Mohammed Mpinga (kulia) akikabidhiwa stika  na Mkurugenzi wa Mawasiliano na  Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia jijini Da res Salaam leo,zitakazotumika katika zoezi la wiki   ya Usalama barabarani inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania itakayofanyika kitaifa mkoani Geita hivi karibuni.
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamanda Mohammed Mpinga (kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na wiki   ya Usalama barabarani itakayofanyika kitaifa mkoani Geita hivi karibuni,wakati wa kukabidhiwa stika zitakazotumika katika zoezi hilo zilizokabidhiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na  Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia(wapili kulia)
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamanda Mohammed Mpinga (wapili kulia)wakipongezana na wadhamini wa wiki ya Usalama barabarani itakayofanyika kitaifa mkoani Geita hivi karibuni wakati wa kukabidhiana stika maalum kwa ajili ya zoezi hilo jijini Dar eS Salaam leo,kutoka kushoto Mkurugenzi wa Mawasiliano na  Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia,Mkurugenzi mkuu wa Puma energy,Philippe Corsaletti na Mkurugenzi wa Selcom,Benjamin Mpamo.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamanda Mohammed Mpinga (kulia)akionesha stika zitakazotumika katika wiki ya Usalama barabarani itakayofanyika kitaifa mkoani Geita hivi karibuni wakati wa kukabidhiana stika hizo maalum kwa ajili ya zoezi hilo leo jijini Dar eS Salaam,wanaoshuhudia kutoka kushoto Mkurugenzi wa Mawasiliano na  Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia,Mkurugenzi mkuu wa Puma energy,Philippe Corsaletti.


Kuna Maoni 4 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Hizi stika miaka nenda miaka rudi sijapata elewa madhumuni yake zaidi ya kibakuli cha mchango kwa ajili ya Polisi. Kwa jinsi Jeshi letu la Polisi linavyokusanya mapato kwa sasa nadhani hii ya kuuziana sticker imepitwa na wakati!!

 2. Anonymous Anasema:

  Hizi sticker kazi yake ni kutafuta pesa kwa Polisi ama ni nini? Naomba kufahamishwa?

 3. Anonymous Anasema:

  Root cause ya ajali nyingi hasa mjini ni ulevi wa madereva.Drink & drive Tanzania ni kama imehalalishwa, ni nadra kuona askari akimsimamisha na kumchukulia hatua dereva mlevi mpaka pale madhara yanapokuwa yametokea.
  Jeshi la polisi inabidi libadilike la maisha ya watanzania yataendelea kuteketea.

 4. Anonymous Anasema:

  stika itakuwa na maana iwapo mwenye kuwa nayo kwenye gari lake hatasumbuliwa kusimamishwa na matrafiki , manaake ni kwamba iwapo trafiki ataona gari lina stika basi hatakiwi kulisimamisha na kulihoji maswali ya uchwara ( triangle, first aid box nk), atatakiwa kulisimamisha gari lisilo na stika na kuuliza maswali yake ( leseni iko wapi, nk)