THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WABUNGE WA SIMBA NA YANGA KUCHEZA MECHI KUCHANGIA WAHANGA WA KAGERA

  Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge William Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika mchezo wao kati ya wabunge wa Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa Septemba 25 katika Uwanja wa Taifa ikiwa na lengo lenye kuchangia wa wahanga wa tetemeko la Ardhi wa wamkoani Kagera, Kulia ni nahodha wa timu ya Bunge, Sixtus Mapunda na kushoto ni Mkurugenzi wa benchi la ufundi Professa Maji marefu.
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azan 'Zungu' akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuelekea Mchezo  utakaochezwa Septemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movie jijini Dar es Salaam leo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanatarajiwa kucheza mechi ikiwa na lengo la kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoa wa Kagera.

Mwenyekiti wa klabu ya Michezo ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, William Ngeleja amesema kuwa mchezo huo utakaochezwa Septemba 25 katika Uwanja wa Taifa utajumuisha wabunge wanaochezea Simba na Yanga.

Ngeleja amesema kuwa, wabunge hao watacheza mchezo huo kwa pamoja ila mwaka huu kumekuwa na sura mpya nyingi sana ambazo mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa lakini lengo kuu ikiwa ni kuchangia wahanga wa Kagera.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azan 'Zungu' amesema kuwa taifa limepata janga la taifa Kwahiyo anawaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuwachangia watanzania wenzetu ambao kwa kipindi hiki wanaishi katika mazingira mabaya.

Viingilio vya mchezo huo utakuwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko kijani na bluu, 10000 na 15000  kwa  viti vya machungwa, VIP A 200,000, VIP B 100,000 na VIP C ni 50,000 huku kutakuwa na viti 50 vilivyotengwa ambapo kwa yoyote atakayekaa hapo atalipia 1,000,000.

Katika siku hiyo pia Kutakuwa na mechi ya mpira wa pete kati ya TBC na wabunnge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanawake huku Wasanii wa  bongo fleva na Bongo Movie.