Na Editha Karlo wa blog ya jamii ,Kagera.

WADAU mbalimbali wanaendelea  kutoa misaada kwa wahanga wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera lililotokea septemba 10 mwaka huu.

Bank ya NMB imetoa msaada kwaajili ya wahanga wa tetemeko wa bando 45 za mabati,tani 20 cementi na misumari mabegi 10 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 20.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Kijuu, Domina Feruzi Mkuu  kitengo cha huduma za kibenki kwa serekali alisema kuwa Bank ya NMB inawapa pole wahanga wote wa tetemeko la ardhi na ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.

"Tunawapa pole waathiriwa na tetemeko la ardhi,tumewaletea msaada huu,lakini tutaendelea kushirikiana zaidi"alisema Domina

Pia  makampuni ya Bakheresa (SSLB) nayo yalikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera vyenye thamani ya shilingi milioni 100.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa SSLB, Tido Muhando alisema kuwa wameguswa na maafa yaliyotokea na hivyo na wao wameamua kutoa msaada kwa wathiriwa hao.

"Tumetoa msaada wa vifaa vya ujenzi na chakula vyenye thamani ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi"alisema Tido

Baada ya kupokea  misaada hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu aliwashukuru kwa misaada hiyo,na kuwataka wadau mbalimbali kuendelea kutoa misaada kwani bado wahanga wanahitaji.


Sehemu ya msaada uliotolewana bank ya NMB kwaajili ya wahanga wa tetemeko Mkoani Kagera
Tido Muhando akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera kabla ya kukabidhi msaada wa wahanga wa tetemeko la ardhi.
Mkuu wa Mkoa akimshukuru Tido Muhando kwa msaada uliotolewa na kampuni ya SSLB kwaajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi.
Mkuu wa kitengo cha huduma za kibenki kwa serekali kutoka NMB makao makuu Domina Feruzi akitoa maelezo kabla ya kukabidhi msaada kwa mkuu wa Mkoa wa Kagera kwaajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nashauri misaada yote ya vifaa vya ujenzi iratibiwe na ofisi ya mkuu wa mkoa na JWTZ, Magereza pamoja na JKT waingie kazini kusaidia ujenzi wa nyumba za waathirika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...