THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAFANYAKAZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WATINGA MAHAKAMANI

Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko.

Na Woinde shizza,Arusha.
Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wamefungua kesi kumshtaki Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kwa madai ya kuvunja mikataba ya ajira.

Kesi hiyo wameifungua katika Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ) kitengo cha awali.

Wafanyakazi watatu kutoka Idara ya Amani na Usalama wanadai Juni 17, Katibu Mkuu huyo alivunja mikataba yao ya ajira kinyume na agizo la Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya

Afrika Mashariki waliyoyatoa kwenye mkutano wa nyongeza wa 31 na kwa kuzingatia Kanuni ya 96 ya taratibu za wafanyakazi wa EAC ya mwaka 2006.

Wanadai kuwa walipokea barua kutoka Masjala ya EAC yenye notisi ya miezi mitatu ya kusitishwa kwa ajira zao iliyowekwa saini na katibu mkuu huyo, huku ikieleza kuwa EAC haina fedha za kuendeleza mradi wa APSA unaopata fungu kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Umoja wa Afrika (AU).