THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAHITIMU 1365 WAMALIZA MAFUNZO YA KIJESHI MLALE JKT, SONGE


 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge wa pili kulia,akikata utepe jana wakati wa uzinduzi wa kituo cha  Internet Cafe katika kikosi cha 842 KJ Mlale kilichopo wilayani Songea,kulia ni mkuu wa kikosi hicho meja Absolomon Shausi. Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Songea Mhe. Palolet Mgema,mwakilishi wa mkuu wa jeshi la Kujenga taifa Kanali John Mbungo na kushoto ni kaimu mkuu wa Brigedi  ya   401 Songea, Meja Absolomon Shausi
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge akikagua gwaride rasmi la vijana 1365 waliojiunga na mafunzo ya  kijeshi ya miezi mitatu katika kikosi cha 842 Kj- Mlale Jkt kwa mujibu wa sheria operesheni Magufuri 2016 kilichopo wilayani Songea
 Baadhi ya vijana  wa operesheni Magufuri 2016 waliojiunga na  mafunzo ya kijeshi ya miezi  mitatu katika kikosi cha 842 Mlale Jkt wakipita kwa mwendo wa kasi mbele ya mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge(hayupo pichani) wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo hayo jana.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge katikati akizindua Jarida la Mlale leo linalochapishwa na kikosi cha 842 KJ Mlale JKT kilichopo katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni kaimu mkuu wa kikosi hicho Meja Absolomon Shausi,wa pili kulia mkuu wa wilaya ya Songea Mhe. Palolet Mgema na mwakilishi wa mkuu wa Jkt Kanal John Mbungo.

 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa baraza la ulinzi na usalama la mkoa wa Ruvuma na maafisa wa mbalimbali wa JWTZ NA JKT mara baada ya kufunga rasmi mafunzo ya kijeshi ya miezi mitatu kwa  vijana 1365. Picha zote na Muhidin Amri